• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RC Dodoma ataka miradi kukamilika kwa wakati na ubora

Tarehe iliyowekwa: November 13th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka mafundi kumaliza ujenzi wa miundombinu ya madarasa kwa wakati na kujenga kwa ubora ili waweze kulipwa malipo yao kwa wakati kwa kuwa fedha za ujenzi wa miradi hiyo zimekwishatolewa.

Ameyasema hayo alipofanya ziara katika eneo la ujenzi wa Shule ya Amali mradi uliopo katika kata ya Kingale na ujenzi wa madarasa 4 na matundu 8 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Dilai hivi karibuni.

Akiongea katika mradi huo Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema miradi ikikamilika kwa wakati itasaidia kufikia malengo ya Serikali ya kuanza kuwapokea wanafunzi na ubora utasaidia majengo hayo kuwepo kwa muda mrefu na kuwasaidia wanafunzi wengi kujifunza na kupata ujuzi.

“Ujenzi wa shule ya Amali umekwishatengeneza ajira mbalimbali kwa wananchi wa Kingale ikiwemo mafundi wanaojenga lakini pia kwa wanawake ambao wamejitokeza kuuza chakula kwa mafunzi hao hali inayoongeza mzunguko wa fedha katika kata hiyo na Wilaya kwa ujumla”amesema Mhe. Rosemary.

Aidha ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo wananchi watapata ujuzi wa vitendo kwa fani mbalimbali ambazo zitakuwa zikitolewa shuleni hapo ikiwemo ufundi cherehani, ufundi uwashi na ufundi wa kuchomelea.

Aidha amewasisitiza vijana na wananchi wote kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika novemba 27 mwaka huu ili waweze kuchagua viongozi watakaowasaidia kuwaletea maendeleo katika mitaa yao.

Hata hivyo ameongea na wanufaika wa mkopo utokanao na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji Kondoa iliyotolewa hivi karibuni ambapo amewaasa kurejesha kwa wakati ili wengine wanufaike na walionunulia pikipiki kuzingatia usalama barabarani na kuepuka kunywa pombe.

Mradi wa Ujenzi wa shule ya amali unagharimu kiasi cha shilingi milioni 544 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa 12 mwaka huu ili uanze kufanya kazi mwezi Januari mwaka 2025.


Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa