• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RC Mahenge azitaka Halmashauri kutatua kero za walemavu kufikia Machi 2020

Tarehe iliyowekwa: December 3rd, 2019

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amezitaka Halmashauri za Mkoa huo kuunda kamati, kufanya sensa kwa watu wenye ulemavu na kuwasilisha taarifa hiyo ofisini kwake ifikapo Machi 30,2020.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota alipokuwa akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa katika maadhimisho ya watu wenye ulemavu kimkoa yaliyofanyika katika uwanja wa Sabasaba Kondoa Mjini.

“Mkoa wa Dodoma baadhi ya Halmashauri zimeunda kamati za watu wenye ulemavu ambapo kwa mitaa ni asilimia 52 na vijiji asilimia 58 hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunaongeza kasi na kufikia asilimia 100,”alisema Dkt. Mahenge.

Aidha alizitaka halmashauri hizo kutenga asilimia 3 za ajira kwa ajili ya watu wenye ulemavu kwani nao wanaweza kufanyakazi kama watu wasio na ulemavu.

“Asilimia 2 ya mikopo imeendelea kutolewa kwa watu wenye ulemavu hivyo ni wakati wao kuchangamkia fursa hiyo ili waondokane na dhana ya kuwa ombaomba na kujiinua kiuchumi,”alisisitiza Dkt. Mahenge.

Hata hivyo aliipongeza Halmashauri ya Mji Kondoa kwa kutoa mikopo kwa vikundi viwili kwa watu wenye ulemavu na kukipongeza chama cha SHIVYAWATA kwa kuunganisha vyama vya watu wenye ulemavu na kuwaweka pamoja.

“Kauli mbiu ya mwaka huu inaendana na hali halisi ya sasa ambapo inahamasisha watu wenye ulemavu kushiriki katika masuala ya uongozi na tumeona Mheshimiwa Rais alivyowateua katika nyadhifa mbalimbali wakimemo Mhe. Stela Ikupa, Balozi Abdala Possi na Naibu Katibu Mkuu Amon Mpanju,”alisema Dkt. Mahenge.

Awali akisoma risala kwa niaba ya watu wenye ulemavu Mkoa wa Dodoma Bwana Justus Ng’wantalima alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa wakalimani wa alama katika taasis za serikali na kutofanyika kwa vikao vya kamati za watu wenye ulemavu katika maeneo yaliyounda kamati..

Maadhimisho ya watu wenye ulemavu duniani hufanyika kila Desemba 3 na kwa mwaka 2019 maadhimisho hayo yamefanyika Wilayani Kondoa ambapo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa serikali na Mashirika binafsi na ilibeba kauli mbiu iliyosema “Kuhamasisha Ushiriki wa watu wenye Ulemavu na Uongozi, Tekeleza malengo ya Maendeleo endelevu ya 

  

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa