• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Serya washukuru kwa bilioni 2 za miradi ya maendeleo kwa miaka minne

Tarehe iliyowekwa: August 31st, 2024

Wananchi wa Kata ya Serya wameishukuru Serikali na Halmashauri ya Mji Kondoa kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika sekta za afya, elimu, maji, umeme, barabara na kilimo na mifugo katika kipindi cha miaka minne.

Hayo yamesemwa na Mheshimiwa diwani wa kaya ya Serya Mhe. Kulwa Pazi alipokuwa akiongea katika mkutano wa wananchi ambao ulioongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kupita kata kwa kata kwa ajili ya kusoma mafanikio ya serikali katika kata zote 8 za Halmashauri ya Mji.

“Kwa kweli serikali imetufanyia mengi makubwa wananchi wa Serya tulikuwa na changamoto za afya imetujengea kituo kikubwa japokuwa kuna changamoto ya kukosekana kwa umeme, pia kwenye elimu tumepokea fedha nyingi kutoka serikalini, Halmashauri na mfuko wa jimbo tunashukuru sana,”amesema Mhe. Pazi

Pamoja na mafanikio hayo yote  ameiomba serikali iwasaidie changamoto ya daraja katika Mto Bubu kwani bado ni changamoto kubwa kwananchi wa Serya msimu wa masika ikiwa ni pamoja na kumaliza changamoto ya mgogoro wa mipaka ya Swagaswaga na wananchi ili waendelee na shughuli zao za kujitafutia kipato.

Akisoma fedha zilizoletwa na Serikali kuu Mtendaji wa Kata ya Serya Ndg. Hamis Juma Amesema katika kipindi cha miaka minne serikali imeleta fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika sekta ya Elimu Msingi milioni 452.5, Elimu Sekondari shilingi milioni 209.5, Elimu Bila Malipo milioni 63.4, Afya ujenzi wa kituo cha Afya Serya milioni 590 na barabara milioni 633.5 ikiwa ni pamoja na kuleta umeme katika mitaa 2.

“Mhe. Mwenyekiti kupitia mapato ya ndani ya Halmshauri ya Mji tumepokea shilingi milioni 56.4 za ujenzi wa zahanati ya Chandimo ambalo lipo hatua ya umaliziaji, mfuko wa jimbo umetuletea shilingi  milioni 11 kwa ajili ya shule shikizi ya Tekule na Serya ambapo wananchi katika miradi yote hii wamechangia shilingi milioni 6,”amsema Mtendaji Hamis

Akiongea katika mkutano huo Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge amewataka wananchi wa kata hiyo kuendelea kuwa na imani na serikali kwani inafanyia kazi changamoto zote za wananchi zilizowasilishwa hivyo ni waoa kuwa na subira.

“Niwapongeze Serya mmepiga hatua kwenye suala la maji kwani katika mitaa yote maji yapo ila nawasihi muitunze tu miundombinu ya maji ili itumike kwa muda mrefu. Aidha kwa upande wa Mto Bubu muendelee kuwa na subira kwani serikali imekwishafanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa daraja hilo muhimu na kiunganishi cha mikoa ya Singida na Kondoa na linahitaji fedha nyingi,”amesema Mhe. Kiberenge

Aidha amewataka wananchi hao kuendelea kuwa na umoja kwani taifa llote ili liendelee linatakiwa kuimarisha umoja na amani kinyume na hapo itatumia muda mwingi kutatua migogoro badala ya kuleta maendeleo kwa wananchi.

“Nawaomba sana wananchi mchangie maendeleo ya Kondoa kwa kutoa ushuru kupitia tozo mbalimbali za kisheria kwa bila kufanya hivyo hatuwezi kuleta maendeleo kwani fedha zinazokusanywa ndizo zinarudi kwaajili ya kujenga vituo vya afya mfano zahanati ya Chandimo inajengwa kwa fedha za mapato ya ndani na hapa tu na maeneo mengine ya Halmashauri,”amesisitiza Mhe. Kiberenge.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa anafanya ziara katika kata 8 za Halmashauri kwa ajili ya kusikiliza kero ya zananchi na kusoma fedha za maendeleo zilizopelekwa kwa wananchi wa kata hizo kwa kipindi cha miaka 4 ambapo Serya ni kata ya pili baada ya Kingale na anaongozana na Wakuu wa Idara na Vitengo na watalaam kutoka taasis zingine za Serikali.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa