• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Shule na Walimu waliofanya vizuri 2024 Kondoa Mji wazawadiwa

Tarehe iliyowekwa: February 20th, 2025

Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari Halmashauri ya Mji Kondoa waliofaulisha wanafunzi kwa alama za juu katika mitihani ya kitaifa wamepewa zawadi ya fedha taslimu ikiwa ni sehemu ya motisha kwao na walimu wengine kufundisha kwa bidii ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi, shule na Halmashauri.

Hafla ya kuwa kuwakabidhi zawadi imeongozwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Ndg. Ally Mbena na imefanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Ualimu hivi karibuni.

Akiongea baada ya kukabidhi zawadi hizo Ndg. Ally Mbena amesema Mkuu wa Wilaya anawapongeza walimu wote waliofanya vizuri na kusema kuwa iwapo wote kwa Pamoja wataenda kutekeleza kwa  mikakati iliyowekwa na mkoa halmashauri inaweza kutoka ilipo na Kwenda mbali zaidi.

“Mkuu wa Wilaya amesema niwaambie kuwa ana ndoto kubwa na Kondoa anataka kama tunavyofanya kwenye mambo mengine na elimu tufanye vizuri zaidi na hataki kuona tunakuwa wanyonge tena kwenye sekta ya elimu”amesema Mbena.

Aidha ameongeza kuwa walimu wanapaswa kutimiza wajibu kwa kuwa haki inaenda na kutimiza wajibu lakini wengi ni wepesi wa kudai haki na wazito kutimiza wajibu hivyo kila mmoja kwa nafasi yake katika ngazi zote kuanzia Halmashauri hadi Mwalimu wa darasani atimize wajibu ili kuona matokeo chanya.

Ameongeza kuwa mwaka 2025 ni wa maelekezo hivyo wanapaswa kutekeleza maazimio ya kikao cha wadau wa elimu mkoa kilichoshauri mambo mbalimbali na kikao cha wadau wa elimu wilaya ambacho kilikubaliana kutengeneza timu ya ufuatiliaji ili kupita katika shule zote na kuona changamoto za mtu mmoja mmoja zitatuliwe kwa wakati.

“Timu hii itasaidia sababu itakapofika katika eneo iangalie kwasababu matatizo yanatofautiana kulingana nae neo nae neo changamoto iliyopo Bolisa haifanani na iliyopo Hachwi unaweza ukafikiri suala la kutoa chakula ndio muarobaini kuna wanaotoa chakula na wanafanya vibaya sababu matatizo yanatofautiana,”amesema Mbena

Akiongea kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge suala la kutoa motisha ni jambo ambalo halmashauri imejiwekea na itaendelea nalo sababu ni agizo la mkoa na wao kama Waheshimiwa Madiwani wataenda kuangalia namna bora zaidi ya kuboresha elimu kwa kuwamotisha na wengine.

“Pia niwashukuru Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu wengine wote kwa kazi kubwa mnayofanya wamezungumza viongozi wenzangu wakati tunaingia madarakani tulikuta shule ina wanafunzi 95 wamepata ufaulu wa 0 lakini sasa wamebakia 6 tusifikiri ni kazi rahisi hii imetokana na umoja wetu kazi ya sisi viongozi na walimu”amesema Mhe. Kiberenge.

Kwa upande wao wawakilishi wa wabunge wamesema kuwa Ofisi zao zitaendelea kuwawezesha walimu kwa kuhakikisha wanazidi kuwamotisha wote waliofanya vizuri kwa kuwanunulia mashine za kudurufu karatasi na kuwapatia fedha taslimu waliofaulisha kwa alama za Daraja A na kuwatia moyo ambao hawajapata zawadi kuwa wana nafasi ya kufanya vizuri nao mwakani na kupata zawadi.

Zaidi ya walimu 50 kutoka Shule za Serikali na binafsi za Msingi na Sekondari wamepatiwa zawadi kwa kufaulisha vizuri katika mitihani ya taifa ya darasa la nne, saba, kidato cha pili na nne pamoja na shule zilizoongeza ufaulu kwa mwaka 2024.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa