• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

SIDO yatoa mafunzo kwa wajasiriamali 60 Kondoa Mji

Tarehe iliyowekwa: January 24th, 2021

Shirika la Viwanda vidogo Tanzania (SIDO) limewajengea uwezo wajasiriamali 60 wa Halmashauri ya Mji Kondoa ili waweze kuboresha biashara zao na kukuza kipato.

Mafunzo hayo yametolewa katika ukumbi wa CCM Kondoa ambapo yalifungwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa hivi karibuni.

Akitoa taarifa fupi kabla ya kufunga mafunzo hayo Afisa Uendelezaji Biashara  kutoka Shirika la SIDO Bwana Crispin Kapinga amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa lengo la kuimarisha biashara za wajasiriamali hao na kuongezea thamani mazao yao ili yaweze kudumu na kumvutia mnunuzi.

“Kwa kipindi hiki cha siku tano tumetoa mafunzo ya vitu mbalimbali kama utengenezaji wa karanga za kusaga, upakiaji wa asali, ufungashaji wa mafuta ya alizeti na utengenezaji wa mikate kwa kutumia unga wa viazi lishe japokuwa hili hatukulifanya kwa vitendo sababu ya muda ila maelekezo tuliyotoa yanatosha watafanya kitu,”amesema Bwana Kapinga

Ameongeza kuwa na mafunzo hayo wameweza kutoa mafunzo ya jinsi ya urasimishaji na usimamiaji wa biashara ambapo wamewajazisha fomu za kuomba bidhaa hizo za wajasiriamali ziweze kutambulika na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambapo wamefanya hivyo kwa kuwa mashirika haya yanafanya kazi kwa kushirikiana lengo likiwa kumpunguzia mlolongo wa kuzunguka mjasiriamali.

Akifunga mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa amewapongeza wajasiriamali walioshiriki katika mafunzo hayo kwani wangeweza kuamua kuwa wavutabangi na kuuza bangi biashara ambayo ni haramu lakini kwakushiriki katika mafunzo ana imani wataboresha biashara zao vizuri.

“Mkumbuke kuwa serikali haitoi fedha za mikopo kwa mtu mmoja mmoja ila kwa vikundi nawashauri mtengeneze vikundi ili mkope fedha nyingi toka Halmashauri zitakazowawezesha kununua mashine kubwa ya kusaga mkapaki unga wa ugali na kuuza maeneo mbalimbali badala ya fedha tunazotoa sasa za milioni moja kwa kikundi ambazo mwisho wa siku tija yake ni kidogo,”amesema Mkurugenzi Dakawa

Ameongeza kuwa vikundi vitakavyoanzishwa viwe na mwelekeo wa viwanda na eneo la kiwanda si lazima liwe kubwa sana kwani hata sasa kuna kiwanda cha kuzalisha gypsum Kondoa ambao wanatumia eneo kubwa hivyo akawasihi washiriki kuwaunga mkono wajasiriamali hao ambao pia walishiriki katika mafunzo hayo.

“Pia nawashauri msiwe wakwepaji wa kulipa kodi ya serikali kwa kulipia leseni za biashara na kununua vitambulisho vya wajasiriamali kwani fedha hizo ndizo zinazoendesha serikali kama utekelezaji wa miradi mikubwa lakini pia ndizo hizohizo zinarudi katika vikundi kwa asilimia kumi na jinsi kodi inavyokusanywa ndio wanufaika wa asilimia 10 wanavyopata fedha zaidi,” amesisitiza Mkurugenzi Dakawa.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Irene Mosha amewashukuru SIDO kwa ujio wao na kuona umuhimu wa kuwajengea uwezo wajasiriamali hao na kuwashukuru kwa kuwaunganisha na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kuwaomba wawasaidie kuwaunganisha na GS One ili wapate Bar Code itakayowezesha bidhaa zao kuuzwa sehemu mbalimbali.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Bahati Machela amesema kuwa mafunzo hayo yamewaongezea uwezo mkubwa na kuahidi kuyafanyia kazi na wengi wataondoka tofauti na walivyokuja na wameishauri Halmashauri kuendelea kuwawezesha mikopo ili ujuzi walioupata usipotee bure na kuwaepusha na kuchukua mikopo yenye riba kubwa.

Jumla ya washiriki 60 kutoka vikundi mbalimbali vya wajasiriamali kutoka Kondoa Mjini walishiriki mafunzo hayo ambapo mwisho walitunukiwa vyeti vya ushiriki mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa CCM Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa