• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Wazee ni hazina" - Mkurugenzi Dakawa

Tarehe iliyowekwa: February 4th, 2021

Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa amesema wazee ni hazina kubwa kwani wao ni miongoni mwa wananchi ambao mchango wao ni muhimu sana kwa taifa na halmashauri  kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa katika hafla ya uzinduzi wa baraza la wazee akimwakilisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kondoa lililofanyika katika ukumbi wa jengo jipya la Halmashauri ya Mji Kondoa hivi karibuni.

“Kila mtu mwenye umri wa miaka 60 na kuendelea anahaki ya kuwa mjumbe kwenye baraza la wazee bila kujali itikadi za vyama, kabila wala dini,”amesema Mkurugenzi Dakawa.

Hata hivyo  Mkurugenzi Dakawa ameishukuru Serikali ya awamu ya tano na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha mpango wa uanzishwaji wa mabaraza ya wazee katika nchi ambao umewezesha upatikanaji wa takwimu sahihi na kwa wakati kuanzia ngazi ya mtaa na Taifa kwa ujumla.

“Serikali imeweza kubaini takwimu  zinazohusiana na  idadi ya wazee kwa ajili ya mipango ya maendeleo, ambapo Halmashauri ya Mji Kondoa inajumla ya wazee 5000 ambao kati yao wazee 4000 wametambuliwa na kupewa vitambulisho  na bado zoezi la upigaji picha wazee linaendelea ambapo kata ya Kingale inaongoza kuwa na idadi kubwa ya wazee kwa asilimia 90”, aliongeza Mkurugenzi Dakawa.

Hali kadhalika Mkurugenzi Dakawa aliendelea kusema kuwa serikali imejitahidi kuhakikisha kuwa upatikanaji wa madawa na huduma za msingi kama vile matibabu bure vinapatikana muda wote kwa ajili ya wazee na kuahidi kufanyia kazi changamoto ya upatikanaji wa dawa.

Naye mwenyekiti mteule wa baraza la wazee Mohamed Yusuph Majala amewaomba viongozi waliochaguliwa pamoja na wazee wote katika  baraza hilo kufanya kazi kwa ushirikiano ili kwa pamoja waweze kutimiza nia ya serikali ya kuwaleta wazee wote pamoja.

“Vijana mna mambo mengi ya kubuni tofauti na sisi wazee tunaishi kwa historia sasa katika kujua mambo mengi sisi hatujui mambo mengi ila tutayajua mambo mengi kupitia kwa wenzangu na vijana hivyo tushirikiane na kupitia mabaraza haya tunaomba tupate miongozo ya jinsi ya kuyaendesha haya mabaraza,”amesisitiza mzee Mohamed

Hafla ya uzinduzi wa baraza la wazee imefanyika ambapo pia wamechagua viongozi wa baraza hilo, lengo ni kuleta mabadiliko makubwa yanayohusiana na wazee kama ilivyo kwa mujibu wa sheria na sera ya wazee ya mwaka 2003 kuhusu uundaji wa mabaraza ya ushauri ya wazee kuanzia ngazi za Mitaa, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Mji Kondoa Msoleni Dakawa akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya  na kuhudhuriwa, baadhi ya wakuu wa Idara na wajumbe wa baraza hilo.




Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa