• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Taa za Barabarani Kubadilisha Muonekano wa Kondoa Mjini

Tarehe iliyowekwa: June 18th, 2018

Mji wa Kondoa unatarajiwa kubadilika kimuonekano baada ya kukamilika kwa uwekaji lami, ujenzi wa makalvati, ujenzi wa mifereji na uwekaji wa taa za barabarani katika barabara za mitaa ya Kondoa Mjini.

Ufafanuzi huo ulitolewa na Kaimu Meneja wa TARURA Kondoa Mji Mhandisi Wera Kweka alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa kazi za TARURA mbele ya wajumbe wa baraza la Halmashauri ya Mji katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

“Fedha zilizotengwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017 zimefanya maboresho katika barabara za mjini kwa kuziwekea lami ambapo kazi inayoendelea ni ukamilishaji wa ujenzi wa mifereji, makalvati na mwisho itakuwa ni uwekaji wa taa za barabarani na jumla ya barabara zilizowekewa lami ni Kilomita 1.2.”Alisema Kweka

Aidha aliongeza kuwa kwa fedha za bajeti ya mwaka 2017/2018 wamejipanga kutengeneza barabara za Mjini yenye jumla ya urefu wa Kilomita 1.26 ambazo zitagharimu kiasi cha zaidi ya milioni miasita na wameshapata mkandarasi na anaendelea na kazi.

Alizitaja barabara hizo kuwa ni Njiapanda-Madiba Kilomita 0.29, Njiapanda-Madiba- Sabasaba Yard Kilomita 0.125, CCM- Tumbero Road Kilomita 0.33, CCM- Iboni Shule ya Msingi Kilomita 0.25 na Tumbero- Soweto kwa Babu Shop Kilomita 0.29.

Aliendelea kutaja barabara zilizofanyiwa matengenezo kwa bajeti ya mwaka 2017/2018 kuwa ni barabara za KKKT, Makaburini, Mashine ya Alizeti na barabara ya Iboni pia fedha hizo zimetumika kuchimba mifereji umbali wa mita 500 na kutengeneza makalvati yenye sentimita 900.

Hatahivyo Mhandisi Wera Kweka alizitaja kazi zinazoendelea kwa kipindi hiki kuwa ni matengenezo ya barabara ya Serya- Mongoroma Mtalyangu yenye urefu wa Kilomita 8 kwa kuijengea makalvati ya “line 3” na kuweka changarawe umbali wa Kilomita 3.

“Pia katika mradi huu zitajengwa kalvati za boksi na kujenga ukuta wa mawe kwa ajili ya kuzuia maji na kazi imeshaanza na jumla ya shilingi milioni mia moja na ishirini zitatumia hadi kukamilika kwa mradi huu.”Alisema Kweka

Maboresho ya barabara zote hizo unafanywa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini Kondoa Mji tangu kuanzishwa kwake mapema mwaka jana.


Matangazo

  • Matokeo ya Kidato cha Sita Kondoa Girls 2025 July 07, 2025
  • Tangazo la kazi za muda June 28, 2025
  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Kondoa Mji yatoa motisha kwa watumishi waliofanya vizuri ukusanyaji wa mapato 2024/2025

    July 08, 2025
  • Kondoa Mji yatoa milioni 90 ya Mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu awamu ya tatu

    July 01, 2025
  • Kondoa Mji watoa mafunzo kwa vikundi 16 vya mikopo awamu ya tatu

    June 24, 2025
  • Wataalam wa Kilimo na Mifugo Kondoa Mji watembelea Nanenane Jijini Dodoma

    June 24, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa