• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Taarifa utazotoa kwa karani ni siri" - Dkt. Mkanachi

Tarehe iliyowekwa: July 30th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamisi Mkanachi amewahakikishia wananchi wa Kondoa kuwa taarifa watakazotoa ni siri kati yao na makarani wa sensa na zitatumika kwa ajili ya kupata takwimu zitakazopelekea serikali kupanga mipango yake na si vinginevyo.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa tamasha la kuhamasisha sensa ya watu na makazi lililofanyika katika uwanja Sabasaba Kondoa Mjini.

"Mkae mkifahamu kuwa taarifa hizi hazitumiki kwa namna yoyote zaidi ya kitakwimu tu kupanga mipango ya kiserikali sawasawa usije ukahofisha sasa ukaanza kudanganya ukajiwekea mambo makubwamakubwa kumbe hayapo au ukafichaficha kumbe vipo utatukwaza kama serikali maana tutashindwa kupanga mipango yetu ya maendeleo kwa watu wetu,"amesema Dkt. Mkanachi

Aidha amewataka washiriki wa bonanza hilo kwenda kutoa ujumbe sahihi juu ya sensa kwa kuelezea maswali yatakayoulizwa siku ya sensa na kuongeza kuwa watakaopita kuchukua taarifa ni makarani wa sensa waliopewa mafunzo ambapo zaidi ya wataalam laki mbili wamepewa mafunzo na kwa Wilaya ya Kondoa ni wataalam zaidi ya elfu moja watashiriki kwa fedha za serikali hivyo jambo hilo ni muhimu kwa kuwa serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji.

"Makarani watakaokuja watakuwa wamevaa sare maalum hawatavaa kama  mimi hapa track suit  na watakuwa na vitambulisho hatakuja mtu kutoka sehemu yoyote na hatakuwa peke yake atakuwa na Mwenyekiti wako wa mtaa au kijiji na watakuwa wamechukua tahadhali zote ya kujikinga na UVIKO 19 kwa hiyo hakuna atakayeambukizwa na atakayemwambukiza karani wetu zoezi litakwenda vizuri na litakamilika,"amesisitiza Dkt. Mkanachi

Naye mbunge wa Kondoa Mjini Mhe. Ally Makoa amesema wananchi wengi wanaelimu ya sensa jambo lililobakia ni kuendelea kutoa elimu kwenye vikao na mikutano ili waendelee kupata elimu na kuongeza kuwa upatikaji wa takwimu hizo utasaidia kupata miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa uendelezaji wa miji TACTIC ambao idadi ya watu ni kigezo muhimu kwa ajili ya kupata miradi hiyo.

Bonanza hilo limefanyika ikiwa ni mwendelezo wa zoezi la kutoa elimu ya sensa ambapo Mkuu wa Wilaya aligawa vipeperushi kwa makundi mbalimbali na kushiriki katika zoezi la ukimbiaji katika maeneo ya mjini na mpira wa mguu  kati ya timu ya Wasafi na Sensa Spesho ambapo timu zote zilifungana goli 2 na lilihudhuriwa na watumishi wa taasisi za ssrikali na wananchi wa wilaya ya Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa