• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Tokeni ofisini mkatoe elimu ya masuala ya ardhi"- Mhe. Angelina Mabula

Tarehe iliyowekwa: September 21st, 2021

Watumishi wa Idara za Ardhi wametakiwa kutoka maofisini na kwenda kwa wananchi kutoa elimu mbalimbali za masuala ya ardhi badala ya kusubiria kwenda kutatua migogoro tu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Angelina Mabula wakati wa kikao kazi na watumishi wa Wilaya ya Kondoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kondoa hivi karibuni.

“Kuna mambo mbalimbali yanayoendelea Wizarani nendeni mkatoe elimu hizo kwa wananchi ikiwemo suala la uhakiki wa umiliki wa taarifa za wamiliki wa ardhi ikiwa ni pamoja na kuwaelezea umuhimu wa wananchi kuwa na hati,”Amesema Mhe. Mabula

Aidha amesema uhakiki wa taarifa za wamiliki wa ardhi utasaidia mmiliki kutopoteza viwanja anavyomiliki kwani kwasasa watu wengi wamepotea viwanja vyao kwa kuandika majina ya watu wengine kwa kuhofia kuonekana na viwanja vingi wakati sheria inamruhusu kumiliki viwanja hata kumi.

“Uhakiki huu utasaidia mmiliki kutumia jina lake moja kwa viwanja vyote maeneo tofauti kwa faida ya vizazi vyake vijavyo na madodoso yatasambazwa nchi nzima ili kujaza taarifa na wakurugenzi nchi nzima nawaagiza kutenga madawati maalum kwa ajili ya kufanyia uhakiki,”amesisitiza Mhe. Mabula

Aliendelea kwa kuagiza maeneo yote ambayo bomba la mafuta litapita Wakurugenzi kutenga fedha kwaajili ya kufanya mpango wa matumizi ya ardhi kabla mradi haujaanza kwani kwa kutoyapanga maeneo hayo yatavamiwa na kuwa hovyo.

“Mgogoro wa King’ang’a inatakiwa pande zote mbili zikutanishwe wote na nyaraka zao na wapima waje kupima mipaka halisi ambayo itakubaliwa na pande zote ili kusiwe na mwingiliano tena kwa kuwa eneo hilo lina maslahi kwa pande zote mbili na lilitolewa kwa nia njema,”amesema  Mhe. Mabula

Akiongea awali Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Dodoma Thadeo Kabonge amesema Wizara kwasasa haipo tayari kupokea migogoro mipya inayoanzishwa na wataalam kizembe kama kuwapangia kiwanja kimoja watu wawili na kuchukua fedha za watu bila kuwapatia hati ambapo  migogoro itakayofanyiwa kazi ni  ile ya kiasili.

“Kuna viwanja vingi vilivyopimwa ila havina hati ongezeni makusanyo kwa kuwaandalia watu hati kwani bado tupo nyuma ambapo kwa mwaka 2020/2021 Halmashauri ya Mji Kondoa ilisajili hati 117 na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ilisajili hati 89 na kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Hamashauri ya Mji wameshasajili hati 30 tukazane kwa kuwa lengo la mkoa ni kusajili hati laki moja,”amesisitiza Kabonge

Naye Mbunge wa Kondoa Mjini  Mhe. Ally Makoa amemuahidi Mhe. Naibu Waziri kuwa atakuwa wa kwanza kuhamasisha wananchi kuchukua hati ili serikali ipate mapato na kuwaagiza wataalam wa Ardhi kuandaa mpango kabambe ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuifanya Halmashauri ya Mji kuwa Manispaa.

Kikao kazi na Mhe. Naibu Waziri kimefanyika ikiwa ni mwendelezo wa vikao anavyofanya nchi nzima ambapo ameongeza mtumishi mmoja katika Idara ya Ardhi Halmashauri ya Mji Kondoa na kilihudhuriwa  na viongozi wa Ardhi mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara na Watendaji wa Kata.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa