• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Tuige uvumilivu wa Mwalimu Nyerere" - Mkurugenzi Dakawa

Tarehe iliyowekwa: October 14th, 2020

Wananchi Halmashauri ya Mji Kondoa na watanzania kwa ujumla wameshauriwa kuiga uvimilivu aliokuwa nao Baba wa Taifa wakati huu ambao nchi ipo katika ujenzi wa miradi mikubwa inayoendelea. 

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa alipokuwa akiongea  wakati wa kongamano la kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililofanyika katika ukumbi wa Shule ya Wasichana Kondoa hivi karibuni.

“Baba wa Taifa alikuwa mvumilivu sana wakati wa kipindi chake cha uongozi alijitoa kwa kila hali pamoja na magumu yote aliyoyapitia kutoka kwa wakoloni lakini hakukata tamaa aliendelea kuitetea nchi ya Tanzania hadi ikapata uhuru,”amesema Mkurugenzi Dakawa

 Aidha ameongeza kuwa kutokana na uvumilivu aliokuwanao ulimpelekea Baba wa Taifa kuwa mzalendo namba moja kwa kuwa alikuwa pia muwajibikaji katika kazi yake ya ualimu kwa kutembea umbali mrefu hadi Pugu Sekondari kufundisha bila kuleta utegezi na visingizio mbalimbali.

 “Kila kiongozi kwa awamu yake amefanya mambo makubwa na ndio maana hata leo tunaona nchi ina maendeleo makubwa sababu Baba wa Taifa hakuwa mbinafsi na Mhe. Magufuli kwa kiasi kikubwa anaendeleza ndoto na maono ya Mwalimu Nyerere ambaye alitamani kuona wananchi wa Tanzania wanaondokana na umaskini na nchi inakua kiuchumi na tumeshuhudia katika awamu hii ya tano nchi imefikia uchumi wa kati,”amesisitiza Mkurugenzi Dakawa

Aliongeza kuwa Raisi kwasasa anatimiza ndoto zilizokuwa za Mwalimu Nyerere kwa kujenga miradi kama mradi mkubwa wa umeme katika mto Ruvu, ujenzi wa barabara, kuhamishia Dodoma makao makuu ya nchi, kutoa elimu bila malipo, kujenga hospitali na vituo vya afya kila wilaya lengo kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za afya bila kutembea umbali mrefu.

“Hata ambao wamejenga nyumba watakubaliana na mimi kuwa wakati wa ujenzi hali hubadilika ndani ya nyumba kwa kubana matumizi ambapo kama ulikuwa unakula nyama kila siku utakula mara moja kwa wiki lakini nyumba ikiisha unaamua hata kuchinja mbuzi ukiwa nyumbani kwako, hata sasa Mhe. Raisi Magufuli anajenga nchi akimaliza kila kitu kitakuwa sawa tuwe wavumilivu,”amesema Dakawa

Akiongea katika kongamano hilo Mkuu wa Shule ya Wasichana Kondoa Mwalimu Frola Nussu amesema shule imemuenzi Mwalimu Nyerere katika falsafa yake ya Elimu ya kujitegemea ambapo wanalima mbaazi ambazo wakiuza wanapata fedha za kutimiza mahitaji yao madogo madogo shuleni.

Hata hivyo mmoja wa watoa mada mzee maarufu Mzee Kova amesema kuwa kuelekea katika uchaguzi mkuu watanzania wanapaswa kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuchagua viongozi bora wanaojua shida zao kwani kura zao ndio maisha yao.

Kongamano la kumuenzi Baba wa Taifa linafanyika kwa mara ya pili katika Shule ya Wasichana Kondoa ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa na kuhudhuriwa pia na viongozi wa dini, wazee maarufu, walimu wastaafu, bodi ya shule, walimu, Afisa Maendeleo ya Jamii na wanafunzi na mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na kusikiliza hotuba mbalimbali za Baba wa Taifa. 

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa