• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Tumshukuru Mhe. Rais kwa kuwapeleka watoto shule"- RC Senyamule

Tarehe iliyowekwa: September 15th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wakazi wa kata ya Bolisa na wanakondoa kwa ujumla kumshukuru Mhe. Rais kwa kuwajengea shule kwa kuhakikisha watoto wote wanaotakiwa kwenda shule wanakwenda shule.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi katika Shule ya Sekonadri Bolisa inayojengwa katika kata hiyo Mtaa wa Poisi baada ya kupokea zaidi ya shilingi milioni 544 kwa ajili ya ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya kata ya Bolisa ambapo hadi sasa zaidi ya shilingi 200 zimetumika.

“Mmepata bahati ya kujengewa shule mpya yenye kila kitu na mwaka huu wilaya ya Kondoa mmebahatika sana kwasababu mnakumbka si muda mrefu mmetoka kuona madarasa ya awali yamejengwa ni mazuri yana michezo ya kuchezea watoto yaani utafikiri sijui mko ulaya bembea na kila kitu,”amesema Mhe. Senyamule

Ameongeza kuwa pia imejengwa shule mpya ya Msingi ya Miningani ambayo imekamilisha majengo yote, ambapo dhamira ya Mhe. Rais ni watoto wa kitanzania wote wapate elimu katika mazingira mazuri yanayofikika ili kusiwe na sababu ya kutoshindwa kwenda shule sababu madarasa yanayojengwa kwasasa ni sawa na ya mjini.

“Lakini nitoe shime kwa wanaBolisa kama Mhe. Rais anafanya hivyo wajibu wetu ni moja kuhakikisha watoto wanaenda shuleni, pili najua suala la utoro kwa mkoa wa Dodoma na wilaya ya Kondoa ni mojawapo wenye watoto watoro kwa wingi hivyo uzuri wa majengo uendane na idadi ya watoto wanaoenda shule,”amesisitiza Mhe. Senyamule

Aidha amesema ili thamani ya majengo iwepo watoto waende shule na kuwataka watendaji wa kata na mitaa kuwachukulia hatua wazazi wa watoto wasioenda shule kwa kuwa sheria ipo wazi kwa mazazi ambaye mtoto wake haendi shuleni na hatua zimeanza kuchukuliwa kwa baadhi ya wazazi ikiwemo kuwatoza faini.

Hata hivyo amewataka wananchi wa eneo hilo kuwa walinzi wa vifaa vya ujenzi ili vifanye kazi iliyokusudiwa  kwa kuwa kukamilika kwa miradi kunafanya nchi kuwa na mafanikio kwa muda mfupi ambapo inatoa fursa ya kufanya mambo mengine ya kimaendeleo kwa kuwa yanachukua muda mrefu.

Kwa upande wake Diwani wa kaya ya Bolisa Mhe. Hajati Ramla Abeid amesema kuwa sekondari ilikuwa kilio kikubwa cha wananchi wa kata yake hivyo wanaomba awafikishie shukrani kwa Mhe. Rais ikiwa ni pamoja na kumshukuru Mhe Mkuu wa Mkoa kwa kufika katika kata yao.

Mkuu wa Mkoa amefanya ziara katika kata ya Bolisa katika Halmashauri ya Mji Kondoa kwa kukagua mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Bolisa ambapo aliambatana na wataalam mbalimbali kutoka ofisi yake, Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Khamis Mkanachi, viongozi wa chama, Kaimu Mkurugenzi na wakuu wa Idara.














Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa