• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Tungufu watakiwa kushikamana ujenzi wa madarasa

Tarehe iliyowekwa: October 14th, 2021

Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Kondoa Hassan Kiseto amewaasa wananchi wa Mtaa wa Tungufu kushikamana katika ujenzi wa maboma ya madarasa Shule ya Msingi Tungufu.

Ushauri huo ameutoa wakati wa kikao cha pamoja na Wananchi hao kilichofanyika katika Ofisi za Mtaa wa Tungufu hivi karibuni.

"Kwa hiyo  mradi ambao mnaendelea nao hapa wa ujenzi wa madarasa mawili  wananchi mnapaswa kushikamana katika kujenga maboma alafu fedha ambazo zimetolewa na serikali zitatumika kwa ajili ya umaliziaji sababu zimeletwa kwa ajili ya umaliziaji",amesema Kiseto.

Ameendelea kwa kusema kuwa kwenye maendeleo hakuna neno kushindwa na kama kuna changamoto ni vyema waziseme ili kujua wanakwama wapi na ndio maana wapo kwa ajili ya  kuwasikiliza ili kero zao ziweze kupatiwa msaada.

"Wakuu wa Idara wamepewa watu wawili kila Kata kama Walezi hivyo basi mimi na Sekela ni walezi wa Kata ya Suruke  pamoja na mitaa yake kupitia kikao hiki tumekuja kujitambulisha hivyo kama kuna jambo ambalo lilikuwa linakwama kufika haraka Halmashauri au kwa Mkuu wa Wilaya basi tupo pamoja na ninyi kuona tunaongeza nguvu ya Mawasiliano baina yenu na Halmashauri", amesisitiza Kiseto.

Halikadhalika ameongeza kuwa kama walezi na wao ni sehemu ya jamii ya Tungufu hivyo kama kutatokea kazi inayohitaji nguvu kazi au michango pamoja na mikutano ya hadhara na wao waitwe ili kuendelea kushikamana vizuri kuliko ilivyo kuwa huko nyuma.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge amesema kuwa bado anaimani na wananchi wa Tungufu kuwa wanataka maendeleo na ndiyo maana wanataka marekebisho yafanyike hivyo amewataka kuendelea kuchangia nguvu kazi huku akiwataka viongozi wanaosimamia ukusanyaji wa fedha hizo kufanya kazi yao kwa uaminifu bila kuacha kuwasomea taarifa za mapato na matumizi na endapo watafanya kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

"Unapoacha kuchangia sio kuwa unajiona mjanja hapana ila unaua maendeleo ya kwenu wenyewe na watoto wenu ndio wanaenda kukaa sehemu mbaya na ukiangalia mvua zinakuja na  majengo hayana uhakika wakiangukiwa itakuwaje na sisi tunashindwa kuishawishi Serikali kuleta fedha nyingine kwa sababu hamjamaliza madarasa ya awali,"amesisitiza Mhe. Kiberenge

Hata hivyo Mhe. Kiberenge amewaambia wananchi wa Tungufu kuwa wasiposimama vizuri kwenye miradi inayojitokeza mendeleo yanayoenda kulala ni yaTungufu na aibu itatokea kwao maana Serikali inaendelea kumwaga fedha nyingi na bado kuna miradi mingi ya kutekeleza lakini wao  bado wameshindwa kukamilisha  mradi  mmoja walionao wakati wenzao wote wamekwisha kamilisha hivyo basi katika jitihada za  kuhakikisha anahamasisha wananchi wanakamilisha mradi huo ametoa kiasi cha shilingi elfu hamsini na kuwaomba wengine kufanya hivyo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Suruke Mhe. Japhari Ganga amewashukuru walezi wa Kata ya Suruke waliofika kusaidia kuhamasisha wananchi katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kuahidi kuwapa ushirikiano.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Mtaa wa Tungufu mmoja wa wananchi waliojitokeza kwenye kikao hicho ametoa changamoto zinazowakabili wakazi hao ikiwemo kutokuwepo na mikutano ya wananchi ambayo inatoa nafasi kwa wananchi kutoa maoni juu  ya shughuli za maendeleo zinazoendelea katika Mtaa wao pamoja na kutokuwepo kwa ushirikiano baina ya wananchi na baadhi ya viongozi.

Kikao cha pamoja baina ya viongozi na Wananchi wa Mtaa wa Tungufu kimefanyika huku kikiwa na lengo la kujadili na kutatua changamoto zinazowakabili katika kukamilisha mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na kuhudhuriwa na Mwenyekiti Halmashauri ya Mji Mhe. Mohamed Kiberenge, Kaimu Mkurugenzi Hassan Kiseto, ,walezi wa Kata ya Suruke, Mtendaji Kata na Mtaa pamoja na Wananchi.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa