• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Tusimamie miradi kwa kesho inayong'ara" - Dkt. Mkanachi

Tarehe iliyowekwa: February 24th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Dkt Khamis Mkanachi  amewaasa wananchi na viongozi wa Halmashauri ya Mji Kondoa kusimamia vizuri fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mkutano wa hadhara pamoja na wananchi na viongozi wa Kondoa Mji uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani hivi karibuni.

"Wajibu wetu sisi ni kusimamia vizuri fedha hizi ambazo Serikali inaleta kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali kwenye maeneo yetu lakini pia nimshukuru Rais wetu Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kuniteua kuwa muwakilishi wake katika Wilaya ya Kondoa ninamuahidi kuisimamia vizuri miradi yote ili  miradi inayojengwa  basi iendane na thamani ya fedha inayotolewa", amesema Dkt. Mkanachi.

Dkt. Mkanachi ameendelea kusema kuwa anajivunia kuwa na timu nzuri ya viongozi na wataalam ambao wote wanazungumza lugha moja na wanapopata changamoto wanazigeuza kuwa fursa na kwa sababu hiyo ndio maana hawakwami.

" Tunapozungumzia maendeleo tunazungumzia watu na sio vitu hivyo ni wajibu wetu sisi kama viongozi ni kutengeneza mazingira mazuri kwa kila mtu bila kujali imani au kazi yake na tunafanya hivyo kwa kuimarisha ulinzi na usalama ili kila mtu afanye shughuli zake kwa amani bila kubugudhiwa na chochote"amesisitiza Dkt. Mkanachi.

Vilevile amewaambia wananchi pamoja na viongozi kuwa mnamo tarehe 8/2/2022 Rais Samia Suluhu Hassan aliongea na wakuu wa Mikoa kuhusiana na anuani za makazi pia anataka mrejesho kila mwisho wa mwezi ili kuona zoezi limefikia wapi lakini pia kutambua changamoto mapema na kuzitafutia ufumbuzi na jana Mhe.Mkuu wa Mkoa alikuwa hapa kwetu kwa ajili ya jambo hilohilo na sisi tunalileta kwenu ili tushirikiane kuona linakamilika kwa wakati.

"Nina imani kubwa kwamba kwamba hatutashindwa na jambo hili na tutakuwa wa kwanza kumaliza zoezi hili na leo tumetangaza nafasi 130  za ajira za muda kwa siku saba haya yote tunafanya ili kuhakikisha kuwa zoezi hili linakwenda kukamilika haraka sana ili tuendelee kunga'ra",amesisitiza DC Mkanachi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe.Mohamed Kiberenge amemshukuru Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato ambapo mpaka sasa Kondoa Mji inatekeleza miradi mbalimbali kwa kutumia mapato yake ya ndani na kwamba hii haijawahi kutokea toka kuanzishwa kwake.

" Mbali na miradi ambayo Halmashauri inaitekeleza lakini pia Serikali bado inaendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mingine mingi ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa,jengo la dharura la hospitali pamoja na vituo vya afya kwa hili naipongeza sana serikali yangu",amesema Mhe.Kiberenge.

Halikadhalika mmoja wa wananchi walioshiriki mkutano huo Mzee Hamidu Hamis Mkoti almaarufu Kadogoo amemuomba Mkuu wa Wilaya kuwasaidia wazee ambao hawana uwezo wa kugharamia matibabu ambapo Dkt. Mkanachi amejibu kwa kuwaambia wazee wote kujitokeza na kukata bima ya CHF iliyoboreshwa kwa gharama ya shilingi 30,000 kwa watu sita kwa mwaka sawa na shilingi 500 kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Mkutano wa hadhara kati ya Mkuu wa Wilaya,Viongozi pamoja na Wananchi umefanyika ambapo wananchi walipata nafasi ya kutoa maoni,kero na kuuliza maswali ambayo yalijibiwa na Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi pamoja na wataalamu wa Idara mbalimbali na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya, Kamati ya Ulinzi na Usalama,Wakuu wa Idara na Vitengo,Watendaji wa Kata na Mitaa na Wananchi.

Matangazo

  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Kondoa Mji watoa mafunzo kwa vikundi 16 vya mikopo awamu ya tatu

    June 24, 2025
  • Wataalam wa Kilimo na Mifugo Kondoa Mji watembelea Nanenane Jijini Dodoma

    June 24, 2025
  • Watumishi watakiwa kuendelea kutoa elimu ya stakabadhi ghalani

    June 23, 2025
  • Baraza Maalum Kondoa Mji lapitisha Sheria ndogo kuimarisha vyanzo vya mapato

    June 20, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa