• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

“Tuunge mkono juhudi za serikali kwa kutunza rasilimali zinazotolewa”- Mhe. Bashe

Tarehe iliyowekwa: January 28th, 2022

Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe ametoa wito kwa wakulima wa zao la alizeti kwa mikoa ya kimkakati kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali kuwekeza katika rasilimali ili zisipotee bure.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao nchini Ndg. Nyasebwa Chimango akimuwakilisha Waziri wa Kilimo Mhe.Bashe wakati  wa uzinduzi wa msimu wa kilimo cha zao la alizeti kitaifa uliofanyika katika Halmashauri ya Mji Kondoa Kata ya Suruke Mtaa wa Mlua hivi karibuni.

“Kampeni ya wizara ya Kilimo ni kuhakikisha kuwa wakulima wa alizeti wanapewa mafunzo endelevu ili waweze kupata mazao yenye ubora na viwango stahiki ambapo leo tumeanza na Kondoa Mji na hatimaye kuwafikia wakulima wote nchi nzima hivyo serikali tunatoa wito muunge mkono jihudi hizi ili zisipotee bure”,amesema Mkurugenzi Nyasebwa

Aidha ameendelea kwa kusema kuwa Wizara imeamua kugawa vifaa kwa maafisa ugani wote vitakavyosaidia kuwafikia wakulima kwa urahisi na kuwataka maafisa ugani kuacha tabia ya kutoonekana kazini kwa kisingizio cha vitendea kazi maana hata Wizara haitavumilia kuona hali hiyo.

“Wizara itatoa vifaa kwa maafisa ugani nchi  nzima hili litafanyika hatua kwa hatua na tutafuatilia kuhakikisha kuwa vinatumika kama inavyokusudiwa na si vinginevyo na atakaebainika kufanya udanganyifu atachukuliwa hatua kali za kisheria kwa sababu lengo la Serikali ni kuhakikisha tunaondoa tatizo la uhaba wa mafuta nchini hivyo basi imani yangu ni kuona tunasimama pamoja katika hili”,amesisitiza Mkurugenzi Nyasebwa

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Dkt. Khamisi Mkanachi amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa wanaunga mkono jihudi za Serikali kama Halmashauri ya Mji Kondoa wamepanda alizeti ekari 90 na kuwataka wakulima wengine kuiga mfano huo na jambo la msingi ni kuendelea kuomba ili mvua zinyeshe.

“Mafunzo tuliyopewa na wataalam wa kilimo ni kwa ajili ya mpango mkakati wa kukuza uzalishaji wa zao la alizeti na kupunguza uhaba wa mafuta ya kula nchini ninaamini mageuzi kwenye kilimo cha alizeti yanawezekana na sisi wanakondoa tunayaanza mageuzi sasa”,ameongeza Dkt. Mkanachi.

Halikadhalika Mkuu wa Wilaya ya ameongeza kuwa asilimia 60 ya wananchi wa Kondoa wanajishughulisha na kilimo cha alizeti hivyo amesema kuwa imekuwa kama bahati na neema kwa wanakondoa wote na kuwataka waitumie fursa hiyo vizuri huku wakishirikiana na maafisa ugani kuanzia ngazi ya kijiji,Mtaa hadi Wilaya ili kuweza kufikia lengo la Kitaifa.

Halikadhalika mkulima na mmiliki wa shamba la mfano la alizeti Bw.Mohamed Joli ameishukuru sana Wizara ya Kilimo kwa kuweza kufanya ziara Mlua na kuchagua shamba lake kuwa shamba la mfano la kupanda zao la alizeti kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo na kuongeza kuwa Mlua itakuwa balozi mzuri wa kuhamasisha wakulima wengine kupanda kisasa.

“Sikuwahi kuwaza wala kutegemea kama siku moja ningefikiwa na ugeni mzito kama huu hii ni baraka kubwa sana na niseme tu najisikia raha sana pia nawaombea Mungu awabariki na awazidishie maarifa waendelee kufanya kazi nzuri ya kuwahudumia  wananchi wote bila upendeleo niwaombe tu wakulima wenzangu tuendelee kufuata ushauri tuliopewa na wataalamu wetu ili tuweze kupata mavuno mengi na mwisho wa siku tuondoe uhaba wa mafuta ya kula nchini kwetu”,amesema Bw.Mohamed Joli.

Mafunzo ya uzinduzi wa msimu wa kilimo cha zao la alizeti kwa mikoa minne ya kipaumbele ambayo ni Simiyu,Manyara, Singida na Dodoma yamefanyika ambapo uzinduzi huo kitaifa umefanyika  Halmashauri ya Mji Kondoa Kata ya Suruke Mtaa wa Mlua.









Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa