• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Uadilifu, uaminifu wasisitizwa kwa wasimamizi wasaidizi na waandikishaji wapigakura

Tarehe iliyowekwa: October 5th, 2019

Tukielekea katika zoezi la uandikishaji wapigakura wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata, mitaa na waandikishaji wameshauriwa kuwa waadilifu na waaminifu ili kukamilisha zoezi la uandikishaji wapigakura kwa uaminifu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa alipokuwa akifungua mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi na waandikishaji wapigakura yaliyofanyika katika ukumbi wa Mcha Kondoa Mjini.

"Zoezi mbele yetu ni gumu na ndio maana halifanyiki mara kwa mara hivyo mkalifanye kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu na naamini mtaweza,"alisema Mkurugenzi Dakawa.

Aliongeza kueleza kuwa serikali imewekeza fedha nyingi katika uchaguzi huu na kuleta fedha za uchaguzi mapema ili kuhakikisha hakuna mkwamo wowote hivyo waitendee haki serikali kwa kulifanikisha kwa umakini zoezi hilo.

Aliendelea kusisitiza kuwa washiriki wote waliochaguliwa kuzingatia watakayoelekezwa na wakufunzi na kuacha kufanya kazi hiyo kwa mazoea kwani uchaguzi wa sasa ni tofauti na wa awali hivyo wazingatie zaidi kanuni zilizopo katika uchaguzi wa mwaka huu.

"Usipoelewa uliza usifanye jambo lolote kwa uelewa wako tu mkafanye kazi kwa kushirikiana ukipata mkwamo uliza kwanza na mwisho wa mafunzo mtapewa namba za wakufunzi wasilianeni nao,"alisisitiza Mkurugenzi Dakawa.

Awali akiongea msimamizi wa uchaguzi Kondoa Mji Mwalimu Hassan Mtamba alisema kuwa wasimamizi wote na waandikishaji waliochaguliwa anaamini watafanyakazi vizuri kwa kuwa ni watumishi wa umma kwa mujibu wa kanuni na wamepitia mchakato mrefu hadi kupatikana kwao.

Zoezi la uandikishaji wapigakura litaanza Oktoba 8 hadi 14, 2019 na jumla ya waandikishaji 62, wasimamizi wasaidizi wilaya 3, kata 8 na mitaa 36 waliapishwa na Hakimu Mkazi Davis Jackson Maimu katika mafunzo hayo.

Matangazo

  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne 2025 Shule za Halmashauri ya Mji Kondoa January 31, 2026
  • Matokeo ya Upimaji Kidato cha Pili 2025 January 10, 2026
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Halmashauri ya Mji Kondoa November 06, 2025
  • Matokeo ya Kidato cha Sita Kondoa Girls 2025 July 07, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Kondoa Mji yatoa mafunzo ya mfumo wa SIS kuimarisha na kuboresha mifumo ya utoaji taarifa

    January 09, 2026
  • Kamati ya Lishe Kondoa Mji yapitia mpango wa bajeti 2026/2027

    December 24, 2025
  • DC Nyangasa afungua kikao cha Baraza la Biashara Wilaya ya Kondoa

    December 17, 2025
  • DC Nyangasa ahimiza ushirikiano na ukusanyaji wa mapato

    December 06, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Ziara ya CMT kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo robo ya kwanza 2025/2026
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa