• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

“Upitishaji wa taarifa ya ufungaji wa hesabu za mwisho uwe endelevu”- Mhe Hamza Mafita

Tarehe iliyowekwa: September 24th, 2019

Wataalam wa Halmashauri ya Mji Kondoa wameshauriwa kuendeleza utaratibu wa kupitisha taarifa ya Ufungaji wa Hesabu za Halmashauri katika vikao vya baraza ili kuondokana na hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa fedha za serikali.

Ushauri huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Hamza Mafita wakati wa kikao cha baraza maalum la kupitia na kupitisha taarifa ya Ufungaji wa Hesabu za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kondoa.

“Toka kuanzishwa kwa halmashauri hii mwaka 2016 hakijawahi kufanyika kikao cha baraza la kupitisha taarifa kama hii na hii ni historia kwa mara ya kwanza natoa pongezi za dhati kwa Mkurugenzi na timu ya Menejimenti kwa kulifanikisha hili ndani ya muda uliopangwa na serikali,”alisema Mhe. Hamza

Akisoma taarifa hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji, Mweka Hazina wa Halmashauri Ndugu Onesmo Mwonga alisema kuwa taarifa ya ufungaji wa hesabu za mwisho za mwaka wa fedha 2018/2019 ulikamilika kwa taarifa zote ambazo ni kitabu Kikuu, kitabu cha sekta ya Maji na kitabu cha sekta ya Afya.

Aliongeza kwa kusoma muhtasari wa ufungaji wa Hesabu za Mwisho ambazo zilionyesha vipengere vya mizania ya hesabu za mwaka 2018/2019, Hesabu za Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019, hesabu za mtiririko wa fedha kwa kipindi cha mwaka 2018/2019 ikiwa na bakaa, mali za halmashauri na uchakavu zilizoingia kwa kipindi hicho na mali za kudumu zilizoongezeka kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na hesabu za usuluhisho wa taarifa ya fedha benki.

“Wakati wa kufunga Hesabu za mwisho za mwaka wa fedha 2018/2019 tarehe 30/06/2019, Halmashauri ya Mji Kondoa ilikuwa na fedha taslimu katika akaunti mbalimbali za halmashauri ambazo zilikuwa kiasi cha Tshs. 2,031,655,024.00,”alifafanua Mweka Hazina Mwonga.

Hata hivyo aliendelea kueleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2018/2019 halmashauri inadai jumla ya Tshs. 183,066.421.00 kutoka kwa watu mbalimbali ikiwemo wakusanya ushuru na taasis mbalimbali na inadaiwa jumla ya Tshs. 1,604,626,114.96 ikiwa ni madeni ya wazabuni, watumishi na malipo ya viwanja.

Baraza maalum la uwasilishaji wa taarifa za Hesabu za Mwisho umefanyika katika Halmashauri ya Mji Kondoa ikiwa ni utekelezaji wa agizo namba 31(1) na 31(7) la Memoranda ya fedha za mwaka 2009 na limehudhuriwa pia na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kondoa. 

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa