• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Usafi wa Hospitali uendelee kuuenzi Muungano"- DC Mkanachi

Tarehe iliyowekwa: April 14th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi amewataka viongozi wa Hospitali ya Mji Kondoa kwa kuendelea na usafi wa hospitali hiyo kama ulivyofanyika wakati wa maadhimisho ya kuelekea siku ya kilele cha miaka 60 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ameyasema hayo wakati akionge na viongozi, watumishi na wananchi waliojitokeza kufanya usafi katika Hospitali ya Mji Kondoa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kuelekea kilele cha miaka 60 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Tukija mwezi ujao tusikute nyasi kama kitalu cha TFS hapana ibaki mandhari nzuri yenye hewa nzuri na bustani nzuri mpaka mgonjwa aone raha kuja hospitali sasa usafi huu uendelee”

Aidha amewaambia kuwa siku ya Jumatatu kutakuwa na dua maalum kwa ajili ya kuliombea taifa itakayofanyika katika viwanja vya Jamhuri Dodoma hivyo anawataka viongozi wote na wananchi kujitokeza ambapo usafiri umeandaliwa kwa watakaotaka kwenda ikiwemo viongozi wa dini.

“Kaulimbinu inasema miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Tumeimarika na kushikamana kwa maendeleo ya taifa letu” kwa hiyo tuendelee kuonyesha mshikamano kuonyesha kweli tumeimarika kwa kwenda pamoja na kurudi pamoja tuendelee kuungana mkono”amesisitiza Dkt. Mkanachi

Aidha ameendelea kuwa tarehe 25/04/2024 kutakuwa na michezo mbalimbali katika uwanja wa Sabasaba kuanzia asubuhi na usiku watapata fursa ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia runinga kubwa itakayokuwepo uwanjani hapo ambapo atalihutubia taifa na sherehe zitamalizika saa 6 usiku.

Akiongea awali Mwenyekiti wa CCM Hayati Hadija Suru amewataka wanafunzi kusoma historia ili wajue maana ya Muungano ambao uliasisiwa na Rais wa Tanganyika Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Zanzibar Hayati Abeid Karume ambao walifanya nchi hii kuwa moja yaani Tanzania.

“Mnaweza kujiuliza kwanini tumeungana yote haya watangulizi wetu walipima mambo mengi sana, usalama wa nchi yetu ni muhimu sana kuliko kitu chochote kikubwa ni amani kwani akija adui akaipiga Zanzibar hatuwezi kuwa salama lakini hadi sasa amani imetawala na CCM tutauunga muungano kwa kila hali,”amesema Mwenyekiti Suru.

Viongozi mbalimbali wamekutana kwa ajili ya kufanya usafi Hospitali ya Mji Kondoa kwa kuongozwa na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi wakuu wa taasisi, waheshimiwa madiwani, wakuu wa idara, watumishi na wananchi ikiwa ni sehemu ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya Muungano wa Tanzania ambapo kaulimbiu inasema miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Tumeimarika na kushikamana kwa maendeleo ya taifa letu”



Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa