• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Vijana Kondoa Mji watakiwa kuchangamkia fursa kujiinua kiuchumi

Tarehe iliyowekwa: February 21st, 2023

Vijana katika Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali za kuwaingizia kipato zinazopatikana katika Halmashauri ya Mji ili waweze kujiinua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.

Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mjini Mhe. Juma Makoa akiwa mgeni rasmi katika kongamano la kutangaza fursa mbalimbali kwa wajasiriamali wa Halmashauri ya Mji Kondoa lililoandaliwa na Divisheni ya Maendeleo ya Jamii na kufanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

“Fursa Kondoa zimeonekana ni nyingi mno na kwasasa tumefunguka kiutalii zaidi ya watalii 5000 wanakuja kwenye kituo cha michoro mapangoni kwa mwaka lakini hakuna mtu hata mmoja anayejishughulisha Kolo wengi ni wageni kutoka maeneo mengine tuamke kama meneja alivyoelezea , tumefungua Mkungunero na inafikika, bonde la Swagaswaga serikali imejenga miundombinu fursa nyingi zipo ila bahati mbaya jinsi ya kuzifikia ndio hatujui,”amesema Mhe. Makoa

 

Aidha ameongeza kuwa serikali imeleta miradi katika kila kata ikiwemo ujenzi wa Zahanati, Vituo vya Afya na madarasa lakini vibarua na mafundi wanaotumika katika kazi hizo ni kutoka nje ya Halmashauri ya Mji jambo ambalo si sahihi kwa kuwa lengo la serikali pia ni kupunguza umaskini kwa wananchi wa eneo husika.

 

“Kulikuwa na vijana walichukuliwa kwa ajili ya kazi ya kuchimba mitaro ya maji walikimbia na hawajui kazi za Serikali zina muda maalum na zinatakiwa zikamilike kwa muda huo Mkanadarasi kweli achukue watu kutoka Songea na vijana wetu wapo hapa tuambiane tu ukweli vijana wetu ni wavivu hawataki kuchangamkia fursa,”amesisitiza Mhe. Makoa.

 

Aidha amewapongeza wanawake wengi waliojitokeza katika kongamano hilo na kusikitishwa na vijana na wanaume kubaki nyuma kushiriki kwenye makongamano kama hayo ambayo yanawafungulia fursa mbalimbali ambazo zitawaongezea kipato na kuwainua kiuchumi na hivyo amewataka wazazi kuendelea kuzungumza na vijana kwa kuwaambia ukweli kuwa waache uvivu.

Akitoa mada wakati wa kongamano hilo Meneja wa kituo cha Michoro ya Mapangoni Kolo Ndg. Zuberi Mabie amewashauri wananchi wa Kolo na Halmashauri ya Mji kwa ujumla kutumia fursa za utalii zilizopo katika kituo hicho ambazo kwasasa zinafanywa na watu kutoka sehemu nyingine.

“Fursa zilizopo Kolo kituoni pale ni nyingi ambazo ni malazi kwa wageni, ngoma za asili, kuongoza wageni kwenye mapango yenye michoro, usafirishaji wa watalii, kuanzisha maduka ya zawadi kwa wageni, kufuma na kushona vikoi, kuanzisha kampuni za kitalii na utoaji wa huduma za kifedha kwa kuwa wageni wengi wanakuja na kadi za benki za nje,”amesema Meneja Zuberi

Akitoa ushuhuda kwa niaba ya wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 katika Halmashauri ya Mji Kondoa Bi. Hawa Hassan ameishukuru serikali kwa kuwapatia mikopo kwa kuwa imebadilisha kwa kiasi kikubwa maisha yao na wameondokana na hali ya utegemezi kama ilivyokuwa awali.

Mfunzo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali na kuwapatia fursa zinzopatikana katika taasis mbalimbali kimefanyika ambapo wataalam kutoka TARURA, Ardhi, Michoro ya Mapangoni na Kilimo walitoa mada za kuonyesha fursa mbalimbali katika taasis hizo na kilihudhuriwa pia na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Wasira aelezea faida za Muungano kwa wananchi wa Kondoa

    April 26, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa