• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Vijiji 2 vilivyovamia hifadhi kufutwa 40 kusalia Dodoma

Tarehe iliyowekwa: October 6th, 2021

Vijiji viwili kati ya vijiji 42 ambavyo vipo katika maeneo ya hifadhi katika mkoa wa Dodoma kufutwa ambapo kati ya hivyo 40 vinavyosalia, vijiji 20 vitabakia na mipaka yake kama ilivyo na vijiji 20 vilivyosalia timu ya wataalam italetwa kufanya tathmini na kujua mipaka itakapowekwa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya Mawaziri nane wanaopita katika maeneo ya migogoro kati ya wananchi na hifadhi katika mkutano na wananchi wa Kijiji cha Bereko Wilaya ya Kondoa hivi karibuni.

“Vijiji viwili vilivyopo katika Wilaya ya Chemba hivyo vitaondoka na wananchi wameishalipwa fidia ili kupisha ujenzi wa bwawa la Farukwa  ambalo litalisha maji katika Jiji la Dodoma na baadhi ya vijiji katika Wilaya ya Chemba na Kondoa,”amesema Mhe. Lukuvi.

Aidha amesema marekebisho yatakayofanywa katika vijiji 20 vitakavyofanyiwa tathmini na wataalam yatakuwa shirikishi ili kuwapimia ardhi inayofanana na mahitaji ya vijiji husika na kuweka alama za mipaka zinazoonekana na yote hayo yametokana na huruma ya Rais Mhe.  Samia Suluhu Hassan kwa mkoa wa Dodoma na ana imani baada ya zoezi hilo kukamilika wananchi hawatavamia tena maeneo yaliyovamiwa.

“Serikali imeamua kuja kufanya tathmini upya ya pori la Mkungunero kwasababu limekuwa na taarifa zinazojichanganya kidogo hivyo tutakuja kuweka mipaka upya na ufanya tathmini upya ili maeneo yote yanayohifadhiwa wananchi wajue na tutafanya shirikishi kwa kushikiana na viongozi wa kuanzia wilaya, mkoa na wananchi wanaozunguka pori hili linaanzia wapi na kuishia wapi na tutaweka mipaka inayoonekana,”amesisitiza Mhe. Lukuvi

Aidha ameahidi kulifanyia kazi suala la familia ya Mzee Gadia ambayo ina mgogoro na Wakala wa Uhifadhi wa Misitu katika sehemu ya ekari nne kati ya kumi ya shamba lao  lililopo katika hifadhi kwa kutuma timu ya wataalam kufanya tathmini ya eneo hilo ambapo awali familia hiyo ilishinda kesi mahakamani na TFS wakakata rufaa.

 Akiongea katika mkutano huo mbunge wa Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amempongeza Mhe. Lukuvi kwa kazi iliyofanyika ambapo kwa Bereko tatizo ni mlima wa Salanka ambao wamekaa nao toka zamani na matatizo yameanza miaka ya karibuni shida kubwa ikiwa ni kukosekana kwa mipaka inayotabirika.

“Ukilima mbaazi mwaka huu zikakubali mpaka unasogezwa, ng’ombe wetu asikatishe tunapigwa faini ambayo hatujawahi kuiona tunahiyo changamoto kubwa kwetu kwa hiyo Mhe.Waziri wa Ardhi tukuombe nafahamu kwenye taarifa umeambiwa kuna nyumba mbili tu siyo tatizo la nyumba mbili ni tatizo la kata sita mipaka haieleweki,”amesema Mhe. Dkt. Ashatu.

Aliendelea kwa kumuomba Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso kuwasaidia wananchi wa Kondoa kupata maji kwani yaliyopo hayatoshi kwani baadhi ya kata hakuna maji kabisa hivyo bilioni mbili zitakazotolewa na serikali wahakikishe wananchi wa Kondoa wanapata maji.

Ziara ya Waheshimiwa Mawaziri imefanyika katika mkoa wa Dodoma ambapo imehitimishwa katika Wilaya ya Kondoa mawaziri saba, Manaibu na Makatibu Wakuu walishiriki kutoka Wizara ya Ardhi, Maji, Mifugo, Maliasili, OR-TAMISEMI, Mazingira ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Anthon Mtaka na Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatuma Mganga na Wilaya iliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Khamis Mkanachi na Wakuu wa Idara wa Halmashauri za Wilaya ya Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Wasira aelezea faida za Muungano kwa wananchi wa Kondoa

    April 26, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa