• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Vikundi vilivyohitimu mikopo asilimia 10 vyaunganishwa na Taasisi za fedha

Tarehe iliyowekwa: April 6th, 2021

Vikundi vilivyonufaika na mikopo itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri wameshauriwa kujiunga na kuanzisha kampuni na viwanda vidogo ili kupata mikopo mikubwa na kujiimarisha kiuchumi.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa wakati wa kikao cha kuwapongeza vikundi vilivyowahi kunufaika na mikopo na kukuza mitaji yao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi za Halmashauri hivi karibuni.

" Mmehitimu nawapongeza sana na nyie mnapaswa mkawe mfano na walezi wa vikundi vilivyoanza kupewa mikopo ili fedha walizopata wasije kupeleka kwenye sherehe ikiwa lengo lake ni kuwekeza ili wakue kiuchumi na kuendeleza familia na inawezekana sababu fedha hizi wanarudisha bila riba,"amesema Mkurugenzi Dakawa

Aidha ameongeza kuwa kwasasa wao wamekuwa kimtaji na mapato yameongezeka hivyo ni wakati wao kulipia leseni ya biashara ambayo wanaweza kuitumia kupata mikopo benki itakayowawezesha kukuza mitaji yao na si kitambulisho cha ujasiriamali kama awali ambacho kitabaki kwa ajili ya wajasiriamali wadogo.

"Fedha mlizokuwa nazo baada ya kumaliza mkopo zitumieni kwenye uwekezaji ikibidi fungueni kampuni au viwanda vidogo ambapo mtaajiri watu wengine nasi kama Halmashauri tutawaongezea mtaji hata milioni 20 kuliko fedha mlizokuwa mnazipata awali kama kikundi,"amesisitiza Mkurugenzi Dakawa

Wakiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Mohamed Kiberenge na Makamu Mwenyekiti Mhe. Besela Maunga wamewapongeza wanufaika hao kwa kufikia hatua hiyo na kuwashauri kuwatumia wataalam wa Halmashauri katika miradi wanayotarajia kuwekeza na biashara wanazotarajia kufungua ili wasijekuwekeza fedha kwenye biashara zisizo na tija.

Mmoja wa wanufaika wa mikopo hiyo Bi. Hawa Chora ameishukuru Halmashauri kwa kuwawezesha fedha na mafunzo mbalimbali kutoka katika mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yamewasaidia kusimamia vizuri miradi yao na kukua kiuchumi.

"Sisi kikundi chetu awali kilianza na ufugaji wa nyuki, tukaingia kwenye kilimo cha alizeti ambapo kwasasa tumejiingiza pia katika kazi ya kutengeneza majiko na maisha yetu kwa kiwango kikubwa yamebadilika nawashauri wataopata na waliopata mikopo hivi karibuni walipe marejesho kwa wakati ili wengine nao wanufaike,"amesisitiza Bi. Hawa

Awali akisoma taarifa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Irene Mosha amesema jumla ya vikundi 25 vimefanikiwa kurejesha mikopo yao vizuri na kukuza mitaji yao ambapo wanatarajia kuongeza mitaji zaidi kwa kukopa benki.

"Nawashukuru sana viongozi mmekuwa bega kwa bega sana katika upatikanaji wa fedha hizi na vikundi hivi vimeshakopa zaidi ya mara mbili na kurejesha fedha zote kwa wakati lakini pia hali ya marejesho kwasasa kwa vikundi  vingine inaendelea vizuri,"amesisitiza Bi. Irene

Halmashauri ya Mji kondoa imefanya kikao cha pamoja na wanufaika hao ikiwa ni pamoja na viongozi wa vikundi vilivyopata mkopo katika robo ya pili kwa mwaka 2020/2021 pamoja na wawakilishi wa Benki za CRDB, NMB na TPB waliotoa elimu ya manufaa na fursa ya mikopo ya benki.





Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa