• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Viongozi watakiwa kuhamasisha wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum

Tarehe iliyowekwa: February 1st, 2024

Viongozi wa CCM na Serikali wametakiwa kushirikiana kufanya hamasa kwenye mikutano ya wazazi ili wawapeleke shule watoto wenye mahitaji maalumu na wapate elimu kama watoto wengine.

Hayo yamesemwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Ndg. Pili Mbaga wakati  wa ziara  iliyofanywa na kamati ya siasa mkoa kukagua mradi wa ujenzi wa mabweni ya watoto wenye mahitaji maalum hivi karibuni.

“Tusiwakatie tamaa watoto wenye mahitaji maalum kwani wanaweza kuja kuwa watu wakubwa kwahiyo niwaombe viongozi wa chama na serikali muendelee kutoa hamasa katika mikutano mnayofanya kwa kukaa na wazazi wenye watoto wa mahitaji maalumu kuwapeleka mashuleni,”amesema Katibu

Ameongeza kwa kumpongeza mwalimu ambaye anawasimamia na kuwafundisha watoto hao wenye mahitaji maalum shuleni hapo kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kuwapandisha watoto watatu wenye ulemavu wa akili kwa kufanya vizuri na kupandishwa madarasa.

‘’Wapo wenye ulemavu wa akili wameanza kufanya vizuri kwahiyo nimpongeze mwalimu pamoja na walimu wote kwa kazi nzuri ambayo mnafanya pia  mtafute mwalimu wa kike ambaye atasaidiana na mwalimu wa kiume kuwasimamia watoto wa kike kwani huyu mwalimu tunamtwisha majukumu ya familiya kwa kuwahudumia watoto wa kike na wa kiume,”amesisitiza Katibu

Aidha ameendelea kwa kumuomba Kaimu Mkurugenzi kufanya mchakato wa kutafuta walimu ambao wataweza kuwafundisha watoto wenye mahitaji maalumu katika shule hiyo na msimamizi ambaye atawasimamia katika usafi mabwenini ili kutunza mazingira shuleni hapo.

Ameongeza kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mradi wa mabweni na Mamlaka ya Elimu Tanzania    kwa kuwaongezea mabweni ya kiume pia wasimamizi kwa usimamizi mzuri wa majengo  na kuwataka yaishe kwa wakati ili watoto waweze kusoma.

Akiongea kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Zainabu Haroub amemshukuru Katibu kwa ujio wake na kutembelea miradi kwani kwa kufanya hivyo kunawasaidia wao kama wasimamizi kupata moyo wa kuendelea kusimamia na kuahidi miradi yote kukamilika kwa wakati na kutoa huduma iliyokusudiwa.

Akisoma taarifa ya mradi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Iboni Mwalimu amesema shule imepokea fedha shilingi milioni 128 kutoka Serikali Kuu kwaajili ya ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum ambapo lina uwezo wa kuchukua watoto 80 kwa wakati mmoja ambapo pia kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania wamepata kiasi cha shilingi milioni 142 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba watoto 120 kwa wakati mmoja.

Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Ndg. Pili Mbanga amefanya ziara ya kukagua miradi katika Halmashauri ya Mji Kondoa ambapo alipata fursa ya kutembelea mradi wa ukarabati wa shule ya Msingi Kondoa wenye thami ya shilingi milioni 180 na mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wenye mahitaji maalum Shule ya Msingi Iboni wenye thamani ya shilingi milioni 128.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa