• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Vyeti vya kuzaliwa ni bure msijinufaishe" - DC Mkanachi

Tarehe iliyowekwa: June 28th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa  Mhe. Khamis Mkanachi amewataka wasajili wasaidizi katika zoezi la utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano kutowatoza fedha zozote wananchi kwa kuwa zoezi hilo linafanyika bure.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa kwaajili wasaidizi yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kondoa.

"Vyeti hivi vinatolewa bure lakini kuna fedha za serikali zimetolewa kufanikisha zoezi na fedha hizo zinatokana na kodi zetu sote tunazotoa serikalini lakini lengo kuu ni kuhakikisha huduma hiyo ya Msingi inapatikana kwa watoto wote nawasihi mkalifanye kwa ufanisi na umakini mkubwa,"amesema Mhe. Mkanachi

Aidha amewataka wasajili hao kuvitunza vitendea kazi walivyopewa ikiwemo simu za mkononi kwa kuwa wana taarifa wengine hutumia simu hizo kwa manufaa yao na kuweka vitu visivyotakiwa jambo ambalo ni kinyume na malengo na watakaokaidi hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.

"Tusiende kuishia katika kusajili tu ila tuhakikishe tuna upload taarifa hizi ili ziende mahali husika kwani vyeti hivi vinatumika pia katika kupata takwimu za watoto zitakazowezesha serikali kupanga mipango ya baadae hivyo mkienda kinyume mjue mmewakosesha haki za msingi watoto," amesisitiza Mhe. Mkanachi

Ameendelea kueleza faida za mtoto kuwa na chetu cha kuzaliwa ni pamoja na kutumika wakati wa usajili shule za Msingi na vyuo, kumsaidia wakati wa umiliki wa ardhi ikiwa ni pamoja na kuthibisha uraia wa mtoto husika na kuwasihi kusikiliza kwa umakini wawezeshaji kwa kuwa ana imani watawaelekeza namna ya kutambua wahusika.

Akiongea awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa amewasihi washiriki kujitoa katika kukamilisha zoezi hilo na kuhakikisha watoto wote walio chini ya miaka mitano wanasajiliwa na kupatiwa vyeti.

Naye mwakilishi wa RITA Mohamed Hassan amesema lengo la mafunzo ni kusogea kwa ukaribu huduma ya vyeti vya kuzaliwa ambapo awali wananchi walisafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika ofisi za Katibu Tawala Wilaya ambapo kwa sasa watapata huduma hiyo kwenye maeneo yao.

Zoezi la utoaji wa vyeti vya kuzaliwa limeanza litaanza rasmi tarehe 29 Juni na kumalizika tarehe 3 Julai 2021 ambapo huduma hii itatolewa katika ofisi za kata, Zahanati, Vituo vya afya na hospitali na Halmashauri ya Mji Kondoa ilijiwekea lengo la kusajili watoto elfu tisa na hadi sasa wanasajili watoto elfu Saba na kubakia na watoto elfu mbili kukamilisha lengo.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa