• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Wafanyabiashara Kondoa jisajilini kanzi data ya EWURA kunufaika na bomba la mafuta"- DC Mkanachi

Tarehe iliyowekwa: February 15th, 2024

Wafanyabiashara wa Wilaya ya Kondoa wametakiwa kujisajili kwenye kanzidata ya EWURA ili kuweza kupata fursa mbalimbali za kutoa huduma katika kambi ya wafanyakazi wa bomba la mafuta iliyo mbioni kuanza.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi wakati wa kikao cha baraza la biashara wilaya ya Kondoa lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

“Awali tulifanya kikao na wafanyabiashara kuwaeleza masuala ya kujisajili katika kanzi data ya EWURA ili wapate fursa za kutoa huduma katika kambi ya bomba la mafuta na muda ukatolewa lakini hadi leo hakuna mfanyabiashara kutoka Kondoa aliyejisajili mi siamini kama hakuna watu wenye uwezo wa kutoa huduma hata ya ulinzi si kweli,”amesema Dkt. Mkanachi

Aidha ameongezea kwa kusema kuwa huduma inayopaswa kutolewa ni ya kiwango cha kimataifa ambapo kuna wataalam abao watakuwa wanapima ubora wa bidhaa na iwapo zimekidhi viwango na kipaumbele kitakuwa kwanza kwa wananchi waliopo karibu na eneo la bomba ambapo kwa Kondoa Mjini ni kata ya Serya.

“Wakazi wa Serya wakishindwa kutoa huduma watafuatiwa wananchi wa Kondoa Mjini wakishindwa ndipo watapewa watu wan je ya Kondoa hivyo tuchangamkie fursa ikiwemo kujisajili kwenye kazi data na atakayepata kama atakuwa wa nje ya Kondoa tutamshawishi anunue kwa wakati wa Kondoa,”amesisitiza Dkt. Mkanachi.

Ameongeza kwa kuwaagiza Maafisa Kilimo na Mifugo wa Halmashauri za Kondoa kwenda kuongea na wakulima wa mbogamboga na wafugaji kuongeza uzalishaji kwani soko litakuwa kubwa kwani mayai, kuku, maziwa na mbogamboga vitahitajika kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge amewakumbusha wananchi wa Kondoa kubadilika na kutumia fursa hiyo ili waweze kusonga mbele kiuchumi na kutumia fursa adhimu iliyoletwa na serikali katika wilaya ya Kondoa.

“Twendeni tukazungumze na wananchi na kujipanga ili kujua tunahitaji kwenda wapi na nakuomba Mkuu wa Wilaya utusaidie katika kuhakikisha tunawabadilisha fikra watu wa Kondoa na kupata fursa zitakazotolewa na uwepo wa bomba la mafuta,”amesema Mhe. Kiberenge

Baraza la biashara limefanyika na limehudhuriwa na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Wilaya ya Kondoa ambapo changamoto mbalimbali zimejadiliwa na kupata ufumbuzi hapohapo na zilizohitaji maamuzi zaidi zimepelekwa kwenye mamlaka husika ikiwemo kupunguza ushuru wa hoteli.


Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa