• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wafanyabiashara Kondoa watakiwa kutumia fursa kukua kiuchumi

Tarehe iliyowekwa: September 3rd, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi amewataka wafanyabiashara wa Wilaya ya Kondoa kutumia fursa mbalimbali zilizopo wilayani humo kwa kuwa mazingira yameboreshwa hali ambayo itawafanya hao wakue kimtaji na kuwa wafanyabiashara wakubwa.

 amefanya kikao na wafanyabiashara wa Wilayani Kondoa kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya masuala ya kodi.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao  na wafanyabiashara, wataalam wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Halmashauri  wilayani humo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

“Bomba la mafuta linakuja tumieni fursa hiyo kwa kuungana pamoja na kufanya vitu kwa pamoja ili muweze kutoa huduma mbalimbali kwa wafanyakazi wa bomba la mafuta ikiwa ni pamoja na kununua gari la kubebea maji taka ambalo hakuna kwasasa mtapata kipato na pia wananchi watahitaji huduma yenu,”amesema Dkt. Mkanachi

Aidha amewasihi kuendelea kuwekeza katika sekta ya utalii kwa kuwa kwa sasa mazingira yameboreshwa katika hifadhi ya Mkungunero ambapo inapokea wageni wanaokuja kwa ajili ya kutalii na wanahitaji sehemu za kupumzika hivyo ni wakati wao kujenga hoteli za kisasa zitakazowavutia na wao kujipatia fedha na kukua kichumi.

Aidha amewataka Mamlaka ya Mapato Tanzania kuacha kuwasumbua wafanyabiashara ili wafanye biashara zao kwa utulivu na kutumia lugha nzuri pindi wanapoenda kukusanya kodi ikiwa ni pamoja na kuwatoza tozo wanazostahiki kulipa.

“TRA najua mna utaratibu wenu wa kutoa elimu hivyo mjipange vizuri na wakati mnakusanya mapato inategemea mnaendaje suala la kutoa fedha si rahisi linahitaji ushawishi sasa kama hauna lugha nzuri ya ushawishi nitakupa hela?Hapana siwezi kutoa fedha hebu twende vizuri tuwashirikishe ili watupe kodi tunazozihitaji,”amesisitiza Dkt. Mkanachi.

Hata hivyo amewataka wawatoze kodi zinazoendana na biashara zao kwani kwa kuwatoza zaidi hawatapata kodi kwa kuwa mfanyabiashara hawatakuwa na fedha zaidi ya wanavyozalisha kwani akiweza leo kwa kesho hataweza hivyo ni jukumu lao kumkuza mfanyabiashara ili baadae waweze kupata kodi zinazotakiwa.

Ameendelea kuwasihi vijana wafanyabiashara kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na Halmashauri kujiendeleza kiuchumi kwa kuwa mikopo hiyo haina riba na kuziagiza Halmashauri kuwakutanisha vijana na kuwasaidia kuandika maandiko ya biashara ili wawe na biashara endelevu za zitakazowakuza na kuwa wafanyabiashara wakubwa.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Paul Sweya amewataka vijana chini ya miaka 35 kujiunga katika vikundi na kuomba mikopo kutoka Halmashauri ambayo inatolewa kila robo mwaka na kuwasisitiza kuwa kwasasa mikopo inatolewa kwa njia ya mtandao na elimu ya jinsi ya kuomba inaendelea kutolewa.

Akitoa elimu ya mlipa kodi Afisa Usimamizi Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania Ndg. Philipo Eliamini amesema kodi wanayopaswa kulipa inatokana na faida ya mauzo kwa mwaka na kila mfanyabiashara analipa kulingana na biashara yake na ndio maana kuna wafanyabiashara wakubwa, kati na wadogo.

“Mfanyabiashara ambaye mauzo yake ni chini ya shilingi milioni nne hawajibiki kulipa kodi TRA anachukuliwa kama mjasiriamali mdogo, mauzo ya milioni nne hadi saba kodi yake ni milioni moja, milioni saba hadi 11 kodi milioni mbili na nusu, milioni kumi na mbili hadi milioni 99 atalipa  asilimia 3.5 ya mauzo yake,”amesema Ndg.Philipo

Kwa upande wao wafanyabiashara wameushukuru uongozi kwa kikao hicho cha kuwakutanisha pamoja ambapo pia wamepata fursa ya kuelezea changamoto zao na wameomba kiwe kinafanyika mara kwa mara na wamefahamu mambo mbalimbali kuhusu ulipaji kodi na umuhimu wake hivyo wataenda kuwa mabalozi kwa wengine katika kulipa kodi.

Kikao cha Mkuu wa Wilaya na wafanyabiashara kimefanyika kwa lengo la kuwakutanisha lakini pia kuwapatia elimu ya mlipa kodi ambapo pia kilihudhuriwa na kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Wakuu wa Idara na baadhi ya Wenyeviti wa Mitaa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa