• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Walimu wa Sekondari Kondoa Mji wapewa vishkwambi

Tarehe iliyowekwa: January 15th, 2023

Walimu wa Shule za Sekondari katika Halmashauri ya Mji Kondoa wamepewa vishkwambi 177 vilivyotolewa na Serikali kuu ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira ya ufundishaji kwa walimu hao.

Hafla ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa ambapo iliongozwa na Afisa Elimu SekondariHalmashauri ya Mji Kondoa Mwalimu Annette Nara na kuhudhuriwa na walimu wote wa Sekondari.

Akiongea katika hafla hiyo Afisa Elimu amesema wametoa vishkwambi hivyo kwa walimu hao ili waende wakavitumie katika kufundishia na kujifunzia ikiwa ni pamoja na kupata mada mbalimbali za kielimukwa njia ya kielektroniki.

“Tuna imani vishkwambi hivi vitawasaidia pia katika kupata vitabu kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania ambavyo vinapatikana kwa nakala laini ambavyo vitawaongezea maarifa wallimu wetu lakini pia vitawasaidia  katika kupitia majarida mbalimbali ya kielimu yatakayowasaidia kuboresha uelewao utakaowaongezea maarifa ya ufundishaji,”amesema Afisa Elimu Nara

Aidha katika hafla hiyo Afisa Elimu alimeongelea suala la taaluma ambapo wamekubaliana na walimu kuhakikisha wanafundisha masomo yao na wanafunzi wanafaulu masomo wanayofundisha na amewapongeza  walimu wa Shule ya Sekondari Dilai kwa kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili na kuwapa moyo walimu waliofeli kuhakikisha wanasahihisha makosa yao na kujipanga upya.

“Walimu mkajitume kila mmoja kwa nafasi yake akafanye jambo na tuwe tayari kujifunza kwa waliofanikiwa achaneni na tabia ya kutanguliza changamoto nyingi angalieni mbele mnaweza mkiamua na muache kuwadharau wakuu wenu wa shule kwani baadhi wamevunjika moyo sababu hamuwaheshimu,”amesisitiza Afisa Elimu

Amewataka kila mmoja kujitafakari namna anavyomtii Mkuu wa Shule na jinsi anavyotekeleza majukumu anayopewa na kiongozi wake na kuwataka kuwa  waadilifu na waaminifu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ili wafikie ndoto zao.

Hata hivyo ametoa wito kwa wazazi kuchangia chakula cha watoto wao shuleni ili wapate chakula cha mchana shuleni na kusoma kwa masaa ya ziada kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu cha watoto wao kwani mwaka jana wazazi wengi hawakuchangia chakula.

Akiongea kwa niaba ya walimu wengine Afisa Elimu kata ya Bolisa Mwalimu Adray Kikoti ameishukuru serikali kwa kuwapatia vishkwambi na wosia wa Afisa Elimu kwa walimu kwa kuwa ana imani maneno yake yatasaidia walimu wengi kubadilika.

Katika hafla hiyo jumla ya vishkwambi 177 vimetolewa kwa Maofisa wa Idara ya Elimu Sekondari, Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule na walimu wote wa Sekondari za Halmashauri ya Mji Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa