• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Waliokopa mikopo ya vijana na wanawake watakiwa kulipa madeni

Tarehe iliyowekwa: May 7th, 2024

Wananchi waliokopa mikopo iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya wanawake na vijana wanatakiwa kurudisha fedha hizo kama makubaliano ya awali yalivyokuwa ili kuepusha Halmashauri kulipa deni hilo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi wakati akiongea katika mkutano wa baraza la madiwani la robo ya tatu lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Kondoa.

“Mwaka huu pia niwakumbushe tuna Mwenge wa Uhuru ambapo tutakimbiza tarehe 30 ambapo tutaupokea Bicha kutoka kwa wenzetu wa Chamwino tukakimbiza Kondoa Mji halafu Kondoa Vijijini lakini jambo moja ambalo ni sharti kwa mwaka huu kuna zile fedha za mkopo kutoka kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kinamama na vijana Kondoa Mji tunadaiwa milioni 32 Mwenge hautapiga hatua hadi risiti ya mikopo ionekane,”amesema Dkt. Mkanachi

Aidha ameitaka Divisheni ya Maendeleo ya Jamii  kuwabainisha wote wanaodaiwa ili wajulikane ikiwa ni pamoja na kuelezwa kiasi wanachodaiwa ili walipe mikopo yao huku akitaka siasa kuwekwa pembeni katika jambo hili na kuhakikisha madeni yote yanakamilishwa kabla Mwenge wa Uhuru haujafika wilayani.

Ameendelea kwa kuwaomba madiwani kuimarisha umoja wao wakati wa kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuhakikisha wanamaliza tofauti zao ndani na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kuacha kuwa sehemu ya kuchochea migogoro ya wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa amesema Mhe. Mohamed Kiberenge amewataka madiwani wa Halmashauri ya Mji Kondoa kuwa wamoja na kushirikiana na viongozi wa mitaa ili kuongoza watu na kuwaweka pamoja na kuepuka kuweka makundi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

“Katika yote yanayoenda kufanyika ushauri wa chama lazima uzingatiwe kwa kuwa kila kinachoenda kufanyika kwasababu sisi tupo chini ya mwamvuli wa Chama Cha Mapinduzi lazima tukubaliane ni jinsi gani tunakwenda kuhakikisha maendeleo ya wananchi yanakwenda kufanikishwa,”amesisitiza Mhe. Kiberenge

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa Mhe. Khadija Suru amewataka Waheshimiwa kwenda kushirikiana katika kutangaza kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi iliyofanywa na serikali ya awamu ya sita kwa kipindi chote cha uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mkutano wa Baraza la Waheshimiwa umefanyika ambapo taarifa za utekelezaji za kamati za kudumu za Uchumi, Mazingira, Fedha na Utawala na UKIMWI kwa kipindi cha robo ya tatu Januari-Machi 2024 zimesomwa na kuhudhuriwa na Wakuu wa Idara na wananchi.

Halmashauri ya Mji Kondoa ni moja ya Halmashauri zilizonufaika na mikopo iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya kuwakopesha vijana na wanawake ambapo ilipata zaidi ya shilingi milioni 40 na kukopesha kwa vikundi ambavyo baadhi havijarejesha hadi sasa na juhudi za kuhakikisha wanalipa mikopo hiyo zinaendelea.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa