• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Waliovamia Swagaswaga Wapewa Siku 14 Kuondoka

Tarehe iliyowekwa: January 8th, 2019

Mkuu wa wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota ametoa siku 14 kwa wananchi wote waliovamia hifadhi  ya pori la akiba la Swagaswaga kuondoka ndani ya hifadhi kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Ameyasema hayo alipokuwa akiongea katika mikutano ya hadhara  na wananchi wa mitaa ya Mongoroma na Serya ili iliyofanyika katika maeneo hayo.

Aliongeza kuwa serikali inayafanya hayo ili kuendelea kuhifadhi rasilimali muhimu zilizomo ndani ya hifadhi hiyo ili ziongezeke na kuongeza idadi ya watalii ambao watakuja kwa wingi kupumzika ndani ya hifadhi baada viongozi mbalimbali kuhamia Dodoma.

“Ni wakati maalum sasa watu waheshimu mipaka ya hifadhi na wasikae ndani ya hifadhi sababu serikali ina mkakati  wake madhubuti wa kuendeleza hifadhi zote kama sehemu ya kuongeza pato la nchi”.Alisema Mhe. Makota

Aliongeza kuwa kaya zote zilizomo ndani ya hifadhi na zinafahamika hivyo ni wakati muafaka kwa wao kuondoka  na kuacha kulima kwa mwaka huu kwani wapo waliokata misitu na kuandaa mashamba.

“Pia kwasasa serikali imefanya utaratibu wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo ya wananchi wanaopakana na hifadhi ambapo kwa sasa wapo katika vijiji vinavyopakana na Tarangire ambapo pia ipo katika wilaya ya Kondoa lengo likiwa ni kuweka matumizi ya kila ardhi husika.”Alifafanua Mhe. Sezaria

Aidha akiuliza kwa niaba ya wananchi wengine Bwana Hassan Juma alitaka kujua wananchi walio ndani ya hifadhi na walishafanyiwa tathmini watalipwa lini sababu wameshaambiwa wahame?

Akijibu meneja wa pori la Swagaswaga Bwana Choya Alex alisema kuwa kuna zoezi lililofanyika ni la kutambua kuna kaya ngapi  ndani ya hifadhi kutokana na maelekezo ya wizara na ilifanyika kama   kama sensa na si uthaminishaji ambao huusisha watu wa kada mbalimbali.

“ Wale walikuwepo kuanzia miaka ya sabini huwezi kumtoa hivyohivyo kuna kanuni na sheria za kufuata kwa hiyo tutapata maelekezo kutoka katika mamlaka husika kujua waliokuwepo kwani taarifa na majina yapo.”Alisisitiza Choya

Notisi hii ya siku kumi na nne inaisha tarehe 22/01/2019 ambapo wananchi wote waliovamia pori la akiba la Swagaswaga wanatakiwa kuondoka na imetolewa na mkuu wa wilaya katika vikao vilivyokaliwa katika mitaa ya Serya na Mongoroma.


Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa