• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wanafunzi watakiwa kuvunja ukimya wanapofanyiwa vitendo vya ukatili

Tarehe iliyowekwa: November 30th, 2022

Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kuongea ukweli pindi wanapofanyiwa vitendo vya aukatili ili kutimiza ndoto zao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Irene Mosha wakati wa ziara ya kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika shule za msingi na sekondari ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

"Watoto mjilinde na mafisi ambao ni watu wabaya wanaovunja haki za watoto kwanza msome kwa bidii kwa kuwa haki ya kusoma iko kwenu ndio maana mnaona serikali inajenga madarasa, imeleta walimu inachinga barabara ili nyie tu msome vizuri, lakini kwasasa watoto wa kiume mnafanya mchezo mbaya wa kulawitiana na hapa shuleni mpo kuanzia sasa muache,"amesema Irene

Ameongeza kuwa wavulana wanaofanyiwa ulawiti madhara hawatayaona kwasasa badala yake ji miaka ya mbele ambapo kitendo hicho kitawafanya wao washindwe kuwa baba bora ikiwa ni pamoja na kutokwa na haja kubwa wakati wote hivi wanapaswa kuacha kufanya vitendo vya ulawiti na kusema wanapofanyiwa.

"Michezo hii mnaifanya pia mnapoenda kuchunga ng'ombe mnawaacha kule nyie mnafanyiana huku acheni na watoto wa kike msikubali kulala na wajomba na kina babu wanawadanganya wanawaingilia na hamsemi semeni ili muokolewe wanachowafanyia ni ukatili mvunje ukimya mseme ukweli mwambieni mtu yoyote kama ni mzazi, mwalimu au mtu mzima yoyote ili awasaidie,"amesisitiza Irene

Aidha amewataka wanafunzi wote wanaoenda kwenye mabanda ya video kuangalia mipira kuacha mara moja kwani wengine wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili huko na kujifunza mambo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na kuacha kutumia simu za kupangusa kwa kuwa si umri sahihi kwao kutumia kwa kuwa wanaweza kujifunza mambo yasiyofaa huko.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Ndg. Ally Mwinyikombo amesema si kubakwa tu ndio vitendo vya ukatili hata kushikwa maziwa, kukonyezwa na kuambiwa na wazazi wasifanye vizuri katika mitihani yao ili wafeli ni ukatili kwani kunawapelekea kukosa nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari hali itakayowapelekea kuwa wategemezi.

"Tumekuja leo kuwapatia elimumili mvijue vitendo vyote vya kikatili mnapofanyiwa waambieni walimu wenu tumewaachia namba zetu za simu ili tuwachukulie hatua wote wznaowafanyia vitendo hivyo kwa lengo la kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa katika jamii, na mjue mkilindwa na nyie mjilinde msifanyiwe vitendo hivyo ili mtimize ndoto zenu hapo baadae,"amesema Mwinyikombo

Hata hivyo amewataka kujilinda ili kuepuka kuambukizwa Virusi vya UKIMWI ambavyo kwasasa imekuwa ni janga kubwa kwa vijana wa umri wa miaka 14 hadi 25 na wengi wanaofanyiwa ukatili wa kingono wanaathirika kwa kiasi kikubwa hali itakayopelekea kukosa vijana wakuliongoza taifa hapo baadae.

Vipeperushi vya ujumbe wa kupinga ukatili na Elimu ya ukatili imetolewa kwa zaidi ya wanafunzi 900 katika shule za sekondari za Dilai na Serya na shule za Msingi za Bolisa, Itiso, Iyoli na Munguri lengo likiwa ni kufikia shule zote za Halmashauri ya Mji Kondoa kwajili ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili duniani ambapo huadhimishwa kuanzia terehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Desemba na mwaka huu imebeba ujumbe usemao "kila uhai una thamani,tokomeza mauaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto."


Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa