• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wanakondoa waaswa kudumisha amani na utulivu

Tarehe iliyowekwa: November 18th, 2023

Wananchi wa Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma wametakiwa kudumisha amani na utulivu kwa kufanya matendo mema na yaliyo na tija kwa Taifa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa Bonanza la Michezo na kuuelezea umma mafanikio ya awamu ya sita ndani ya Wilaya ya Kondoa liliondaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt .Khamis Mkanachi na kufanyika katika viwanja vya Sabasaba Wilayani Kondoa.

"Nitoe Shime tuendelee kuimarisha Amani na Utulivu pia tuendelee kufanya matendo mema ambayo yatapelekea nchi Yetu ya Tanzania Kuendelea kuwa na Amani kwasababu Rais wetu ametamani tupendane, tushikamane na tuwe na umoja na ameanza kuyafanya, kupishana kwenye jambo sio kufarakana mnapopishana  mkae mezani kuangalia chanzo cha tatizo na kulimaliza Kama Watanzania," amesema Senyamule

Aidha amewaambia wanakondoa kuwa katika mkoa wa Dodoma Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja 2022/23 amejenga jumla ya shule 47 mpya ikiwa ni jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa awali na uwepo wa shule hizo kutasaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza kiwango cha elimu Tanzania.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Khamis Mkanachi amebainisha kuwa licha ya Bonanza Hilo kujikita katika kuelezea na kuonyesha mafanikio hayo ya awamu ya Sita pia ametaka Bonanza Hilo litumike Kama uwanja wa wanafunzi kumfahamu vizuri Dkt. Samia kwani ni tunu ya Taifa.

Aidha Dkt. Mkanachi ameweka bayana kuwa katika kipindi cha Miaka 3 ya Rais Samia madarakani Wilaya ya Kondoa imepokea Billioni 52.634 za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo na yenye tija kwa Wananchi wa Wilaya hiyo.

Bonanza la michezo limefanyika kwa lengo la kuujulisha umma wa Kondoa mafanikio ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo pia ilifanyika ikiwemo mpira wa miguu,kukimbiza kuku, kukuna nazi, kutembea ndani ya magunia, kuvuta kamba na shindano la kula pilipili na matembezi ya hisani yaliyoanzia katika Barabara ya Darajani Hadi viwanja vya Saba Saba Kondoa Mjini.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa