• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi Kingale wapongezwa kujitolea ujenzi wa miradi ya maendeleo

Tarehe iliyowekwa: July 29th, 2024

Wananchi wa kata ya Kingale katika Halmashauri ya Mji Kondoa wamepongezwa kwa jitihada zao za dhati za kujitoa katika kuchangia miradi ya maendeleo ambapo wamekuwa wakijenga madarasa katika shule za msingi hali inayoonesha jinsi wanavyounga mkono juhudi za uletaji wa fedha za maendeleo unaofanywa na Serikali.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge alipokuwa akiongea na wananchi wa Kata ya Kondoa Katika mkutano wa kusoma utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi cha miaka minne katika kata hiyo.

“Kazi yangu mimi ni kuhakikisha nawaunganisha wanakondoa na wanahalmashauri ya mji kuelewa umuhimu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo lakini kuwaelekeza namna serikali yetu inavyofanya kazi na jinsi inavyoshusha fedha ambazo zipo katika makundi matatu ambayo ni fedha za Serikali Kuu, wahisani na mapato ya ndani”amesema Mhe. Kiberenge

Ameendelea kueleza kuwa kwa kipindi cha miaka minne kwa kushirikiana na viongozi waliopo madarakani wameona fedha zilizoletwa ambazo zimelenga katika kutatua changamoto za wanaKingale katika sekta ya afya, elimu, maji na umeme japokuwa changamoto zipo chache na zinaendelea kufanyiwa kazi.

Amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu fedha za utekelezaji wa maendeleo kuletwa katika kata ya Kingale kwa lengo la kuwasogezea huduma kwa karibu wananchi na kuwahakikishia wananchi hao kuwa fedha hizo zitaendelea kusimamiwa na kutumiwa kama ilivyopangwa hivyo wawe na imani na baraza la Madiwani katika usimamizi.

Akiongea awali Kaimu Afisa Mipango Ndg. Agnes Chekani amesema kwa kipindi cha miaka minne Serikali imeleta shilingi bilioni 2 za maendeleo katika kata ya Kingale ambazo zilielekezwa katika barabara, maji, umeme, ukamilishaji wa zahanati ya Tampori, Ujenzi wa madarasa, vyoo na Maabara Dilai Sekondari, ujenzi wa madarasa Shule ya Msingi Kingale na Iyoli ambapo kwasasa zimeletwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa Shule ya Msingi Chemchem na Dilai Sekondari.

“Pili nataka niwapongeze wana Kingale pia kwa kujitolea kujenga madarasa Kingale Chini, Shule Shikizi Msui na Kwamtwara mna nia ya kujitolea na mwaka huu tutaleta fedha milioni 197 kwaajili ya kukamilisha madarasa ambayo mliiyanzisha katika mitaa ya Kwamtwara, King’ang’a’,Tampori, Msui na Kingale Chini japokuwa tumeshaleta shilingi milioni 5 kwa ajili ya kupaua wa madarasa yaliyojengwa,”amesema Kaimu Afisa Mipango

Aidha ameongeza kuwa Serikali imeleta zaidi ya shilingi milioni 540 kwa ajili ya kujenga shule ya ufundi ili watoto wanaomaliza shule wajiunge na kupata ujuzi mbalimbali utakaosaidia kujitegemea kwa pamoja ambapo shule ya Sekondari Dilai itakuwa ya kidato cha tano na sita.

Pia wananchi walipata fursa ya kuongea ambapo waliishukuru Serikali kwa kuwaletea fedha nyingi katika kata yao nakuomba kumaliziwa umeme mitaa michache iliyobakia na kusaidia kupatikana na kwa walimu kwa kuwa shule zipo nyingi ambapo kwasasa wanawalipa walimu wa kujitolea katika baadhi ya shule ili kuhakikisha watoto wao wanapata elimu stahiki.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mwalimu Hassan Mtamba amewapongeza wazazi kwa kujitolea kuwalipa walimu wanajitolea na kuahidi kuleta walimu kadri serikali inavyowaleta ili kuondoa tatizo hilo ambapo serikali inafanya kila jitihada za kuhakikisha walimu wanaajiriwa na kusambazwa katika shule zote.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa ameanza ziara ya siku 8 ya kusoma utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi wa kata 8 ambapo pia ameongozana na wataalam mbalimbali kutoka Halmashauri ya Mji Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa