• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi Mtaa wa Tampori wajitolea kujenga Zahanati

Tarehe iliyowekwa: July 29th, 2019

Wananchi wa Mtaa wa Tampori kata ya Kingale wamekubaliana kwa kauli moja kujenga Zahanati ili kuepukana na adha wanayoipata katika kutafuta huduma za matibabu wakati wa masika.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mheshimiwa diwani wa kata hiyo na kuwasirikisha wataalam kutoka Halmashauri ya Mji mkutano uliofanyika katika mtaa huo hivi karibuni.

Akiongea mmoja wa wananchi wa kata hiyo Bwana Selemani Said alisema kuwa wananchi wa mtaa huo wana shauku kubwa ya maendeleo hivyo wako tayari kujenga Zahanati ingawa wanachangamoto ya kukosekana kwa umeme na barabara watasubiri kwa kuwa Zahanati ina umuhimu kwao kwa sasa.

“Wananchi wa Tampori tunapata sana shida wakati wa masika tunakuwa kama tupo kisiwani tunapohitaji huduma za afya sababu mito yote hufurika maji mtufikirie sana katika hilo tupo tayari kuchangia nguvu zetu zote na tumeshatenga eneo la ekari saba kwajili ya ujenzi.” Alisisitiza Bwana Selemani.

Kwa upande wake Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji Kondoa Kaunga Amani aliwashukuru wananchi kwa kujitoa kwao na kuahidi kuwaunga mkono wananchi hao ili kuhakikisha ujenzi unaanza hadi unakamilika na kuwataka agenda ya ujenzi iwe ya kudumu kila mahali.

“Wiki ijayo nitakuja na Mhandisi Ujenzi, Afisa Ardhi na Mganga Mkuu ili kuona eneo lililotengwa na kupimwa , baadae tutapata mchanganuo wa fedha zinazohitajika kukamilisha mradi na utaitishwa mkutano wa kupanga kiasi ambacho kila mwananchi atatakiwa kuchangia.”Alisema Kaunga

Alisisitiza kuwa ili mradi ukamilike wananchi watatakiwa kuchagua kamati ya ujenzi na wakumbuke kuchagua wajumbe waaminifu na waadilifu na kufungua akaunti ikiwa ni pamoja na kusoma mapato na matumizi ya mradi kila mwezi.

Kwa upande wake Mheshimiwa wa kata hiyo Abushehe Mbuva aliwaambia wananchi hao kuwa watakuwa pamoja katika kukamilisha mradi huo na kuahidi kumpeleka Mheshimiwa mbunge ili ajionee changamoto inayowakabili wananchi wake.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Wasira aelezea faida za Muungano kwa wananchi wa Kondoa

    April 26, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa