• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Wananchi wahamasishwe kujitolea nguvu kazi"- Mhe. Kiberenge

Tarehe iliyowekwa: October 28th, 2021

Na. Leah Joseph

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe.Abdi Kiberenge amewashauri Viongozi wanaosimamia miradi ya maendeleo kuendelea kuwashawishi wananchi kujitolea nguvu kazi ili kufikia malengo.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mkutano wa baraza la wazi la waheshimiwa madiwani  la kupokea taarifa kutoka kamati za kudumu za Halmshauri uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kondoa hivi karibuni.

"Halmashauri imeendelea kupokea fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo miradi iliyokuwa ikitekelezwa katika Shule za Msingi Bolisa, Ubembeni, Iboni,Shule ya Sekondari Kwapakacha na Bicha imekamilika na inaendelea kutoa huduma zilizokusudiwa hivyo basi ili kufikia hatua kama hiyo ni lazima wananchi washirikishwe toka mwanzo mwa miradi,"amesema Mhe. Kiberenge.

Mhe.Mwenyekiti ameendelea kwa kuwapongeza  wale wote waliosimamia miradi yao vizuri kwa kuhamasisha wananchi kuchangia nguvu kazi ikiwemo Shule ya Msingi Ubembeni na Shule ya Sekondari Ula na kusema wanastahili pongezi kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Halikadhalika kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Paul Sweya amesema kuwa jukumu la Halmashauri ni kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wa Kondoa Mji kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya Serikali.

Mkurugenzi ameendelea kwa kusema kuwa katika kutekeleza majukumu hayo yote inahitajika nguvu ya pamoja katika usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika hatua zote za utekelezaji kwa kushirikiana na timu nzima ya wataalam ambapo kwa sasa kila  Mkuu wa Idara amepewa Kata ya kufuatilia kwa karibu na kutoa taarifa za shughuli zote za maendeleo zinazoendelea katika kata husika.

Hata hivyo akiongea awali Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Hamisi Mkanachi  amewashukuru wote wanaoendelea  kupokea chanjo ya UVIKO 19 na kuwasihi wengine ambao bado kufanya hivyo kwa usalama wa afya zao na za wengine.

Naye Mratibu wa Elimu ya Afya kwa umma Mkoa wa Dodoma Dkt Nassoro Ally Matuzya amesema kuwa Halmashauri ya Mji Kondoa imefanya vizuri sana katika zoezi la chanjo awamu ya kwanza lakini kwa awamu ya pili bado idadi hairidhishi kwa watu wanaochanja.

"Nashindwa kuelewa tunakwama wapi maana Rais wetu Samia Suluhu Hassan pamoja na kuleta chanjo tena kwa gharama kubwa  bado ana nia ya dhati ya kulinda afya za wananchi wake kwani ameongeza fedha katika  miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kupunguza msongamano", ameongeza Dkt Nassoro.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa Mohamed Kova amewasihi viongozi ,wananchi pamoja na watumishi wote bila kujali nafasi zao kudumisha umoja na mshikamano ili kuweza kufanikisha shughuli za maendeleo kwani utengano huleta mpasuko na mgawanyiko hivyo ni vyema wakazika tofauti zao binafsi mahala pa kazi na kuhudumia wananchi.

Mkutano wa baraza la waheshimiwa madiwani wa kupokea taarifa kutoka kamati za kudumu za Halmashauri robo ya kwanza umefanyika na  umehudhuriwa na Mkuu Wilaya,Waheshimiwa madiwani,Kamati ya ulinzi na usalama, Wakuu wa Idara na vitengo, wawakilishi kutoka taasisi za Serikali pamoja na wananchi.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa