• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi Waomba Huduma ya Umeme

Tarehe iliyowekwa: August 18th, 2018

Wananchi wa mitaa ya Bolisa, Ukunku na Mulua wamemuomba mbunge wa Kondoa Mjini kuwasaidia kupata huduma ya umeme katika mitaa yao ambayo imepitiwa na nguzo za umeme wa REA  ili waweze kuboresha maisha yao.

Maombi hayo waliyatoa katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika mitaa hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi iliyofanywa na Mbunge wa Kondoa Mjini Mhe. Edwin Sannda hivi karibuni.

“Mheshimiwa mbunge umeme huku kwetu lini utafika tunaona tu nguzo zimepita na nyaya zake nai umeishia katika mitaa ya jirani tusaidie tupate umeme ili tuanzishe viwanda vidogo vidogo na kuunga mkono juhudi za serikali na kujiongezea kipato? Aliuliza Bwana Mohamed mkazi wa Bolisa

Aidha ombi hili lilikaziwa na wakazi wa Mtaa wa Mlua ambapo walisema ni kipindi kirefu wamekaa bila ya kuwa na umeme na wamechoka kwasasa wanaomba wapate huduma ya umeme.

Akijibu maombi hayo kwa nyakati na meneo tofauti mbunge wa Kondoa Mjini Mheshimiwa Edwin Sannda alisema kuwa serikali imepanga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya umeme na mkandarasi wa kusambaza umeme mitaa ya Kondoa amepatikana kinachosubiriwa ni kuanza kazi baada ya kumaliza Chamwino na Bahi.

“Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kutoa huduma hii na ndio maana inafanya kwa awamu ambapo awamu ya kwanza kuna maeneo yalipata huduma mengine hayakumalizika ikaanza awamu ya pili ambayo ilikamilisha sehemu iliyobakia awamu ya kwanza na kuanzisha miradi mipya na sasa tuna REA awamu ya tatu ambapo inakuja kukamilisha miradi iliyobakia awamu ya pili na kuanzisha maeneo mengine na mitaa yetu ipo humo tuwe na subira tu.”Alisema Sannda

Alidha aliwasihi wananchi kuendelea kutunza vigingi vilivyowekwa na shirika la umeme kama alama za kuweka nguzo kwani maeneo mengine wananchi wamekuwa wakiviharibu na kuwapa kazi wakandarasi wanapoanza kazi na kuwataka kuendelea kufanya maandalizi ya kusuka nyaya za umeme na fedha za kulipia huduma ya kuingiza umeme katika nyumba zao.

Ziara ya mbunge imefanyika katika kata zote nane za Halmashauri ya Mji Kondoa ambapo miradi mbalimbali ilikaguliwa na kufanya mikutano ya hadhara ambapo wananchi walipata fursa ya kuuliza maswali ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka miwili na aliongozana na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa na wataalam kutoa halmashauri ya Mji Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa