• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wanawake Kondoa Mji watoa Bima za Afya kwa watoto yatima

Tarehe iliyowekwa: March 5th, 2024

Wanawake wa Halmashauri ya Mji Kondoa wametoa kadi 154 za bima ya afya iliyoboreshwa kwa watoto na wazee wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto hao vya Mtakatibu Gema na Bicha.

Kadi hizo zimetolewa na Ndg. Christina Kalekezi Katibu Tawala Wilaya ya Kondoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika vituo hivyo akiwa ameambatana na wanawake wa Kondoa waliochangia kuwezesha kupatikana kwa kadi hizo.

“Huu ni utu na ukishakuwa na utu utafahamu kwamba kuna mahitaji mbalimbali ya watoto sisi akina mama ndi tunaojenga taifa ukiona taifa imara lenye viongozi imara kama Dkt. Samia Suluhu Hassan ukimuona namna alivyo na diplomasia na utu na anavyojitahidi kuhakikisha Tanzania iko salama yule mama aliyemlea anapaswa apewe maua yake,”amesema Katibu Tawala

Aidha amesema amevutiwa na utu walioonesha wanawake hao baada ya kuona wameguswa na watoto wanaoishi katika vituo hivyo ambao wanaonekana hawana wazazi lakini wao ndio wazazi wao ka kuwa wamekuwa wakifika mara kwa mara kituoni hapo na kutoa mahitaji mbalimbali ya watoto lakini wameguswa zaidi kwa kuona suala la afya ndilo la msingi.

“Nyie wakina mama mmenishangaza sana kwamba mnapokuwepo hapa afya zinateteleka wengine wanakimbia kwenye baridi wanapata shida mkaona wanavyopata shida wanapataje dawa hawa walezi waliojitolea niwashukuru na niwapongeze kwa kuwa mnaisaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,”amesisitiza Katibu Tawala

Ameongeza kwa kuwapongeza kwaniaba ya serikali na kusema kuwa sasa ndio kwanza wameanza kwa kutoa bima za afya hivyo waendelee kuwalea watoto ili wakue katika misingi na kuwa kama wanawake viongozi kwa kuwa kwasasa kumekuwa na mmomonyoko wa maadili ikiwemo kujiingiza katika vitendo visivyo na maadili.

Akishukuru kwa niaba ya wazee na watoto wa kituoni cha Gema Sista Jane Fransisca amesema anawashukuru wanawake wa Kondoa kwa upendo, umoja  na ushirikiano wao kwa kuwaletea vyote walivyoviandaa ikiwa ni pamoja na bima za afya na kuwaomba kuendelea kuwatembelea katika kituo hicho.

Wanawake wa Kondoa kwa kushirikiana na Halmashauri wametoa michango yao zaidi ya shilingi laki 7 na kutoa bima za afya kwa watoto 154 wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Gema na Bicha Islamic ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8 itakayofanyika kimkoa wilayani Chamwino na kaulimbiu ya mwaka huu inasema “Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii.”

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • "Sintamzibia ruhusa mtumishi anayetaka kwenda masomoni"- Mkurugenzi Majaliwa

    June 01, 2025
  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa