• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Wanawake ni jeshi kubwa lenye silaha zote"- DC Nyangasa

Tarehe iliyowekwa: March 5th, 2025

Wanawake wametakiwa kutambua kuwa wao ni jeshi kubwa na lenye silaha zote hivyo wajiamini kusaidiana, kuinuana na kuungana mkono ili kufikia malengo wanayojiwekea.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa wakati akiongea na wanawake  wa Kondoa Mji wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake katika Halmashauri ya Mji Kondoa katika Ukumbi wa Kondoa Irangi.

"Tuwe na roho ya kuombeana mema sababu tabia ya kuona mwanamke mwenzako amefanikiwa unakasirika ni tabia yako binafsi wewe kwani sisi kama wanawake tuna kila sababu ya kuishi pamoja na hakuna kinachoshindikana"amesema Mhe. Nyangasa

Aidha amesema yupo tayari kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wa Kondoa lakini amewasihi wawe tayari na kuridhika na maamuzi yatakayotolewa wanapoleta jambo kwake kwa kuwa jambo lolote lina  majibu ya aina mbili.

Ameongeza kwa kuwasihi wanawake kuendelea kumuombea Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ameleta miradi ya kutosha Kondoa katika nyanja zote muhimu ikiwemo afya, elimu na barabara.

"Ameleta fedha tunajenga shule ya amali Kingale, shule mpya 16, zahanati na ukarabati mkubwa wa hospitali ya Mji ukiacha miradi ya kimkakati ya kitaifa kama reli ya SGR sasa tumlipe kwa kufanya kazi na shughuli za kiuchumi"amesisitiza Mhe. Nyangasa

Ameendelea kwa kuwataka kuwaunga mkono waheshimiwa madiwani wanawake ikiwa ni pamoja na kuwashawishi vijana kushiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kondoa Mhe. Hija Suru amewataka wanawake kusimama imara kwa kuwa wanaweza wakipewa nafasi kwa kuwa wanajiamini na kukisimamia wanachokiamini.

"Wanawake tujitoe kama wanavyojitoa kikundi cha Wanawake na Samia na nawaombs tuongeze upendo nisemee ninaposemwa mimi vibaya kama sipo na tusemeane mema" amesisitiza Mhe. Suru

Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Halmashauri ya Mji Kondoa zimepambwa kwa maandamano na kugawa mahitaji kwa vituo vitatu vya kulelea watoto Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa