• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wanufaika mikopo ya Halmashauri wapewa mafunzo

Tarehe iliyowekwa: November 3rd, 2022

Wanufaika wa mikopo itokanayo na asilimia kumi ya mapato ya Halmashauri ya Mji Kondoa wamepatiwa mafunzo ya namna ya kufanya biashara zao ili mikopo waliyopatiwa iwe na tija na kuwainua kiuchumi.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Kondoa na kuhudhuriwa na wanavikundi waliopata mkopo kwa robo ya kwanza, Idara ya Maendeleo ya Jamii na wawakilishi wa Kitengo cha Sheria.

Akitoa mada katika mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Kondoa Mjini Ndg. Paschal Materu amewaambia wanufaika hao kuwa wabunifu katika biashara zao wanazofanya ili kujiongezea soko na kuacha kufanya kazi kimazoea hali itayowapelekea kukimbiwa na wateja wao na kujiona biashara wanayofanya haina tija kwao na kushindwa kufanya marejesho ikiwa ni pamoja na kuendelea kudidimia kiuchumi.

“Lazima unapofanya kazi zako ujiwekee malengo na ujiamini na huwezi kujiamini kama unatoa bidhaa mbovu ndio maana nimekuambia wale washindani wako unatakiwa uangalie wapi wanapofeli wewe ndio unaboresha wote tunashona nguo lakini ushonaji wangu na wako unatakiwa utofautiane hata kama mnauza bei moja wa kwako ukiwa bora lazima watu watakuja kwako hata kama utaongeza bei.”amesema Ngd. Paschal

Aidha amewataka kuwa na uhitaji wa mafanikio kutokana na wanachofanya na kile wanachotamani kufikia siku zijazo kutokana na faida anayoipata ikiwa ni pamoja na kwa tayari kuibeba hasara kwani kwa kuogopa kubeba hasara hawawezi kuwa wajasiriamali wazuri hivyo wawe wanaweka akiba kwa ajili ya kuitumia inapotokea hasara.

 Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Ndg. Latipha Koshuma amewataka wanavikundi hao kuwa makini wakati wa ununuzi wa mashine walizoomba kununua kwa kuepuka kununua vitu mtandaoni kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kupoteza fedha kwa kuwalipa watu wasiowajua na kukosa mashine.

“Mnatakiwa kuchagua watu wawili kwa ajili yakwenda Dodoma au Dar kulingana na mashine mnazotaka nendeni moja kwa moja dukani mkaombe profoma na invoice halafu mrudi kuwaonyesha wanakikundi wengine na awape akaunti namba ya benki mfanye malipo halafu awatumie mashine zetu msifanye vitu ndani ya box yaani online itawapotezea muda na mnatakiwa kuwa makini,”amesema Ndg. Latipha.

Hata hivyo amewataka wanavikundi kuwa waaminifu wakati wa marejesho ukifika kwa kuleta fedha kwa wakati na kiwango kilichopo kwenye mkataba ili fedha hizo zitumike kuwakopesha wengine wenye mahitaji na kabla hawajarejesha wanapaswa kufika katika ofisi za Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kupewa kumbukumbu namba ya malipo na wanaopaswa kurejesha ni wanakikundi wenyewe si mtu mwingine.

Mmoja wa wanakikundi Ndg. Hadija Ntisi ameishukuru Halmashauri ya Mji kwa kuwapatia mkopo kwa kuwa ni mara ya pili anapata mkopo ambao umekuwa ni msaada mkubwa kwake na familia yake na kwasasa amiliki kibanda cha kuuza vitu vidogo vidogo  ambapo fedha anazozipata zinamsaidia kujikimu yeye na familia ya kwa ujumla

Jumla ya viwili vimepatiwa mkopo ambapo kimoja ni cha wanawake na kimoja cha vijana na mtu mwenye ulemavu mmoja wamepatiwa mkopo katika robo ya kwanza mwaka wa fedha 2022/2023 na shilingi milioni 11 zimetolewa na wamepewa mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa kuwafundisha mada mbalimbali ikiwemo ujasiriamali na bisahara, mitaji na mikopo, utunzaji wa kumbukumbu ikiwa ni pamoja na kuwasainisha mikataba kati yao na Halmashauri.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa