• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Watakaopata daraja la Kwanza Kondoa Girls kujazwa fedha

Tarehe iliyowekwa: January 23rd, 2021

Wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Wasichana Kondoa wamehaidiwa kupewa shilingi laki tano kwa kila mwanafunzi atakayepata ufaulu wa daraja la kwanza kwa pointi 1 hadi 5 katika mtihani wa utahimilifu mkoa unaotarajia kuanza Februari mosi 2021.

Ahadi hiyo ameitoa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa alipokuwa akiongea na wanafunzi hao katika ukumbi wa shule hiyo hivi karibuni.

"Watakaopata daraja la kwanza pointi 1-5 nitampa kila mmoja shilingi laki tano na watakaopata daraja la kwanza pointi 6-9 nitampa kila mmoja shilingi elfu 20 kwa kuwa najua mkifanya vizuri mtihani huu ni rahisi kufanya vizuri mtihani wa kitaifa," amesema Mkurugenzi Dakawa

Ameongeza kusema kuwa ana imani na wanafunzi kuwa watafanya vizuri kwani miaka yote shule hiyo imekiwa ikifanya vizuri na hata kwani hata matokeo ya mwaka jana hakuna mwanafunzi aliyepata daraja sifuri na ni wanafunzi wachache sana walipata daraja la nne.

"Najua siku za kuanza mtihani zimebakia chache ila mkikazana kusoma mtafaulu japokuwa wanasema ng'ombe hanenepi siku ya mnada ila anashiba hivyo mkikazana katika siku hizo chache zilizobakia mtashiba kwa kufanya vizuri,"amesisitiza Mkurugenzi Dakawa

Aidha amewaambia kuwa itakuwa aibu wanafunzi waliopo Kondoa kushindwa kwenda katika vyuo vikuu vilivyopo Dodoma kama Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu cha Mipango lakini pia shule za mkoa wa Dodoma zinapaswa kuwa kinara kwa kuwa ndio makao makuu ya nchi.

"Niwaombe pia mshirikiane katika masomo mnapoona mwenzenu mmoja anatetereka wakati wa kusoma muiteni mkalisheni chini na mfundisheni ili wote mfaulu maisha mazuri ni kusaidiana na kubebana sidhani kama mtajisikia vizuri kuona wenzenu wanafeli naamini nafsi zitawasuta,"amesema Mkurugenzi Dakawa

Akitoa shukrani Mkuu wa Shule Mwalimu Frola Nussu amesema wamefarijika na ujio wa Mkurugenzi na wakuu wa Idara na wanafunzi walishaahidi kupata daraja la kwanza kabla hajaenda hivyo kwa maneno yake watazidisha juhudi na kumuomba Mwenyezi Mungu awapatie afya njema wakati wote wa mitihani.

Kwa upande wao wanafunzi Getrude Gadau na Tekla Ngalawa wamemshukuru Mkurugenzi kwa kuongea nao na kusema kuwa hawakutegemea kama kiongozi kama huyo angewajali hivyo na kumuahidi kufanya vizuri zaidi.

Mkurugenzi amefanya ziara shuleni hapo kwa ajili ya kuwatia moyo wanafunzi wa kidato cha sita 276 wanaotarajia kufanya mtihani wa utahimilifu mkoa kuanzia Februari Mosi ambapo aliongozana na Afisa Elimu Sekondari na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa