• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Watendaji kusanyeni mapato" - Mkurugenzi Dakawa

Tarehe iliyowekwa: January 8th, 2020

Watendaji wa Kata na Mitaa wametakiwa kuhakikisha wanakusanya mapato katika maeneo yao na kuwatolea taarifa watu wote wanaowakwamisha katika ukusanyaji wa mapato.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa wakati wa kikao cha kawaida cha uboreshaji utendaji kazi kati ya Mkurugenzi, Wakuu wa Idara na watendaji wa Kata na Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Uuguzi Kondoa.

“Mkashirikiane na viongozi wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa kuhakikisha mapato yanakusanywa, nyie ni viongozi msome sheria mbalimbali zinazowaongoza na mzisimamie na muachane na kutumia mashine za kukusanyia mapato nje ya matumizi yaliyokusudiuwa kwani kufanya hivyo ni kosa kubwa,”alisema Mkurugenzi Dakawa.

Aidha aliwapongeza watendaji waliofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwa mwezi Desemba na kumuagiza Afisa Utumishi kumuandalia kiasi cha Shilingi laki moja Mtendaji wa Mtaa wa Kolo A Bi. Mary Baraka kutokana na kukusanya mapato makubwa kuliko watendaji wote kwa mwezi Desemba.

“Kuweni wabunifu wa vyanzo vya mapato na muandae sheria ndogo za maeneo yenu kwani itawasaidia kuongeza mapato yatakayopelekea na nyie kupata gawio kubwa zaidi kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zenu za kila siku,”alisisitiza Mkurugenzi Dakawa.

Aliendelea kuwasihi kuendelea kufanyakazi kwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni ikiwa ni pamoja na kufika kazini kwa wakati na kuheshimu kazi kwani wote watapimwa kwa kazi walizozifanya na kujiepusha kutumiwa na watu wenye fedha kwani kwa kufanya hivyo watageuzwa kuwa watumwa wao.

Akiongea katika kikao hicho Kaimu Afisa Elimu Bi. Annete Narra aliwataka watendaji hao kushirikiana na viongozi walioteuliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaripoti shuleni na kuanza masomo.

“Mwamko wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza bado hauridhishi ni jukumu lenu kuhakikisha waliopo majumbani wanafika shuleni ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wazazi umuhimu wa elimu na kuachana na mawazo ya kuwapeleka watoto wao nchini Oman kufanya kazi za ndani,”alisisitiza Mwalimu Narra

Hata hivyo Kaimu Afisa Mazingira aliwasisitiza watendaji kusimamia shughuli za uzibuaji mitaro hasa kipindi cha mvua, uchomaji wa mkaa maeneo ya makazi ya watu na usafi wa mwisho wa mwezi.

Matangazo

  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Kondoa Mji watoa mafunzo kwa vikundi 16 vya mikopo awamu ya tatu

    June 24, 2025
  • Wataalam wa Kilimo na Mifugo Kondoa Mji watembelea Nanenane Jijini Dodoma

    June 24, 2025
  • Watumishi watakiwa kuendelea kutoa elimu ya stakabadhi ghalani

    June 23, 2025
  • Baraza Maalum Kondoa Mji lapitisha Sheria ndogo kuimarisha vyanzo vya mapato

    June 20, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa