• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Watendaji watakiwa kuwasaidia walengwa wa TASAF kupata stahiki zao

Tarehe iliyowekwa: May 20th, 2024

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Said Majaliwa amewataka Watendaji wa Kata na Mitaa kuwasaidia walengwa wa TASAF kupata stahiki zao wanazolipwa kila mwezi kwa kuwatafuta popote walipo.

Ameyasema hayo wakati wa kikao cha pamoja na walengwa wa TASAF wa mtaa wa Miningani alichoitisha kwaajili ya kusikiliza changamoto za walengwa hao kilichofanyika katika Ofisi ya Mtaa wa Miningani.

“Nawaomba wataalamu wangu hasa watendaji siku ya kugawa fedha umia kuwa kwanini huyu mtu wangu hajapata fedha isiwe kirahisi kumtoa mtu, si ndio Mtendaji hawa ni watu wako sababu leo mtu wako kalipwa dirisha lingine hayupo usitulie nipigie simu kujua sababu za kutoonekana kwa jina lake siyo kwenye vikao kama hivi.”amesema Mkurugenzi Majaliwa

Aidha amewataka kuwafikia walengwa ambao hawafiki wakati wa mgao kwa kuwa wakati mwingine mlengwa anashindwa kufika kutokana na kukosa nauli au kuwa mgonjwa na si kurudisha fedha zake kwa kuwa lengo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ni kuhakikisha walengwa wote wanapata fedha hizo ili kuwasaidia katika kutatua changamoto zao.

Ameendelea kuwahakikishia kuwa hakuna fedha ambazo zimeliwa na watendaji ila ni kukosekana kwa mawasiliano na elimu kabla ya kugawa fedha na kuwahakikishia walengwa wote wa Mtaa wa Miningani waliofanya kazi na kustahili kulipwa fedha kuwa watalipwa fedha zote kwa siku walizofanya kazi.

Hata hivyo amewataka waratibu wa TASAF kuhakikisha wanaitumia siku yote ya Jumanne kwa kufika katika Mtaa wa Miningani na kuwasikiliza walengwa wote wenye changamoto na kuhakikisha wanazitatua na kwa walengwa ambao changamoto zao hazijatatuliwa wafike katika ofisi yake au kumpigia simu ili kuzitatua.

Ametumia fursa hiyo kuwakumbusha walengwa kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi wa serikali za mitaa na maboresho ya daftari la wapiga kura hivyo wajiandae kuboresha taarifa zao ili waweze kuchagua viongozi watakaosaidia kutatua kero zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Miningani Mhe. Ibrahimu Hamisi amemshukuru Mkurugenzi kwa kufika na kuwasikiliza walengwa hao ambao walikuwa na sintofahamu kutokana na kufanya kazi bila kupewa malipo yao.

Mkurugenzi ameeitisha kikao hicho kutokana na kupokea malalamiko kutoka kwa walengwa hao baada ya malipo ya dirisha la mwezi Januari na Februali ambapo baadhi yao hawajapata fedha ikiwa ni sehemu ya kutekeleza kauli ya mkoa wa Dodoma ya Kero yako, Wajibu wangu.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa