• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Waziri Kairuki ampongeza mwekezaji Kondoa

Tarehe iliyowekwa: May 21st, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki amempongeza Bwana Muhammad Mavere mwekezaji wa kiwanda cha mafuta ya alizeti kilichopo katika Halmashauri ya Mji Kondoa kwa kukumbuka kurudi nyumbani na kufanya uwekezaji mkubwa hali itakayowapa moyo wawekezaji wengine kuja kuwekeza Kondoa.

Pongezi hizo amezitoa wakati wa ziara yake katika kiwanda cha Magin LTD aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuona kazi zinazofanyika na kujua changamoto anazokabiliana nazo ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa kongamano la uwekezaji lililofanyika mkoani Dodoma mwaka jana.

“Niwapongeze uongozi wa Wilaya kwa kumlea na kumsaidia mwekezaji huyu lakini niwasihi sana tuzidi kumlea na serikali inawalinda wawekezaji wa ndani kama hawa kwa uwapa moyo hasa wawekezaji katika mafuta ya kula kwani kwasasa serikali inatumia zaidi ya shilingi bilioni 443 kwa kuagiza mafuta nje ya nchi fedha ambazo zingeokolewa na kutoa huduma kwa wananchi wengine,”alisema Mhe. Kairuki

Aidha Mhe. Kairuki alizidi kumpongeza Mwekezaji huyo kwa kuongeza ukubwa wa kiwanda chake tofauti ana awali na kujenga mitambo kwa ajili ya kukamua mashudu na kuwaomba halmashauri kumwongezea eneo lingine na kumsaidia kulipima ili apanue kiwanda chake hali itakayokuza kiwanda na kuongeza ajira kwa wananchi.

“Nawashauri kuchukua mkopo katika taasisi za fedha kwa ajili ya kununua mitambo mikubwa zaidi kwa ajili ya kusafisha mafuta mengi zaidi na kuachana na kwenda kwa wawekezaji wengine kusafisha mafuta kwa kuwa na mitambo yenu mtakua kibiashara na kuongeza uzalishaji,”alisisitiza Mhe. Kairuki

Hata hivyo amemuahidi mwekezaji huyo kuzifanyia kazi changamoto alizokumbana nazo wakati wa kuingiza nchini mtambo wa kukamua alizeti na kupelekea kulipa kiasi cha shilingi milioni 60 ambapo hadi sasa sehemu ya mtambo huo umekwama bandarini kutokana na kutolipiwa ikiwa uingizaji wa mtambo huo hautakiwi kulipiwa kiasi chochote cha fedha.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota amemshukuru Mhe. Kairuki kwa kufanya ziara katika wilaya ya Kondoa na kumpongeza Bwana Muhammad Mavere kwa kuongeza uzalishaji kutoka kuzalisha tani 24 kwa siku alipoanza hadi kufikia tani 50 kwa siku na kumuahidi kutatua changamoto zinazomkabili zilizopo ndani ya uwezo wake na kuziwasilisha sehemu husika zilizo nje ya uwezo wake.

Naye Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Kanda ya kati Bwana Revocatus Rasheli amemsihi Bwana Mavere kuwasilisha changamoto zake katika kituo hicho Dodoma Mjini na kusema kuwa kwasasa serikali imeanzisha vituo vya uwekezaji ambapo mwekezaji atapata huduma zote za serikali katika kituo kimoja anapotaka kuwekeza na kwasasa kituo hicho kipo Dar Es Salaam na kipo mbioni kuanzishwa mkoani Dodoma lengo likiwa ni kuboresha huduma za uwekezaji nchini.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa