• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Waziri wa Ulinzi awaasa SUMA JKT

Tarehe iliyowekwa: October 23rd, 2018

Kampuni ya SUMA JKT inayomilikiwa jeshi la kujenga taifa imetakiwa kutimiza malengo ya serikali ya kujenga majengo yenye ubora na kumaliza kwa wakati ili kundelea kuaminiwa na serikali.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Ulinzi Mhe. Dkt. Hussen Mwinyi alipokuwa akiongea na viongozi wa wilaya ya Kondoa katika ofisi ya Mkuu wa wilaya baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri ya Mji kondoa linalojengwa na SUMA JKT.

Alisema kuwa serikali imewaamini SUMA JKT ambapo kwa sasa wana miradi mingi katika maeneo mengi hivyo ni jukumu la viongozi wa JKT kusimamia miradi hiyo kwa ukamilifu na kuhakikisha inakamilika kwa wakati ili huduma za msingi zianze kutolewa katika ofisi hizo.

“Najua mpo nyuma ya muda wa kazi ila naamini mtafidia kama mlivyoahidi na nashauri mvua zipo karibu mjitahidi kupeleka eneo la kazi vifaa vyote muhimu vitakavyotumika hapo mbeleni ili kuepusha kusimama kwa kazi tena.”Alisisitiza Dkt. Mwinyi

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota alieleza kuwa hana mashaka na kazi inayoendelea kwani anajua SUMA JKT  kazi zao ni za uhakika na viwango na anaridhika na kasi wanayokwenda nayo japokuwa hapo awali walikumbana na changamoto ya barabara ya kwenda kwenye mradi ambapo kwasasa imekwishatatuliwa.

Ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na SUMA JKT inafanywa na Dkt. Mwinyi kwa lengo la kuangalia shuhuli zinazofanywa, changamoto zinazoikabili miradi na kukaa na pande mbili kuona namna ya kuzitatua ambapo katika wilaya ya Kondoa wanajenga jengo la utawala la halmashauri ya Mji ambalo linagharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 ambapo aliongozana pia na Mkuu wa JKT  Meja Jenerali Martini Busungu na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT Kanali Rajabu Mabele.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa