• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wenyeviti wa Mitaa watakiwa kuwatumikia wananchi

Tarehe iliyowekwa: November 30th, 2019

Viongozi walioteuliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni katika Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kutambua kuwa wameteuliwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si wananchi kuwatumikia wao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa wakati wa zoezi la kuwaapisha viongozi hao lililofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

"Nawapongeza kwa kuteuliwa kwenu ila nawashauri msiende kuwa miungu watu na wakali kwa wananchi pia mkaonyeshe ushirikiano kwa watendaji na wataalam katika maeneo yenu ili kurahisisha utendaji kazi na kuleta maendeleo kwa wananchi,"alisema Mkurugenzi Dakawa.

Aidha zliongeza kuwa viongozi hao wanapaswa kwenda kuhakikisha kuwa wanakusanya mapato kwa kushirikiana na viongozi wengine kwani kwa jinsi watakavyokusanya fedha nyingi ndivyo watakavyopata asilimia 20 kubwa zaidi na kuwaletea maendeleo wananchi.

"Mkafanye kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ili kuepuka kuingilia majukumu ya wengine na kurahisisha utendaji kazi na kubwa kwenu  ni kutatua migogoro ya wananchi na wajumbe mkawashauri vizuri wenyeviti wenu,"alisisitiza Mkurugenzi Dakawa.

Hata hivyo aliwataka Watendaji wa Mitaa kushirikiana na wenyeviti wao na wajumbe walioteuliwa kuhakikisha hadi kufikia mwezi Machi 2020 wawe wameandaa mpango wa ujenzi wa ofisi zao za mitaa.

Naye Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Kondoa Michael Sanga aliwasihi viongozi hao kupeleka kwa Watendaji wa Kata au Mitaa makosa ya jinai ili wayashughulikie kisheria na kuepuka kukaa na fedha walizokusanya katika nyumba zao.

Awali akitoa taarifa ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kondoa Msimamizi wa uchaguzi Mwalimu Hassan Mtamba alisema kuwa jumla ya Wenyeviti 36, Wajumbe mchanganyiko 108, na Wajumbe Viti maalum 71 waliteuliwa baada ya kupita bila kupingwa na wote wametokana na Chama Cha Mapinduzi.

Zoezi la uapishaji viongozi hao limefanyika pamoja na utoaji semina elekezi kwa viongozi hao kutoka kwa wakuu wa Idara na ilihudhuriwa pia na watendaji wa Mitaa na waliapishwa na Hakimu Elizabeth Justine kutoka Mahakama ya Wilaya ya Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa