• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ZIARA YA RC MPWAPWA

Tarehe iliyowekwa: November 10th, 2017

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge amewataka watumishi wa Umma na Taasisi mbalimbali kwenye Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kuwahudumia Wananchi kikamilifu na kwa uadilifu wakitambua kuwa sasa Mkoa wa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi hivyo tunayo dhamana kubwa Wanadodoma kuwa mfano kwenye masuala yote ya maendeleo kama Elimu, Afya, Kilimo, Uwekezaji, Viwanda na Biashara na tutumie fursa ya kuwa jirani na Serikali katika kusukuma mbele masuala ya Maendeleo kwenye Mkoa.

Dkt. Mahenge amebainisha kuwa tayari amekutana na kuzungumza na makundi mbalimbali kwenye Mkoa yakiwemo ya Wazee, Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Wafanyabiashara na Wakuu wa Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu ambapo amekutana na Malalamiko ya baadhi ya watumishi kutokuwa waadilifu na kutotekeleza wajibu wao ipasavyo wa kuwahudumia wananchi.

Akiwa Wilayani Mpwapwa jana wakati wa ziara yake ya kutembelea Wilaya za Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kujitambulisha Dkt. Mahenge amesema yapo baadhi ya maeneo Mkoa bado haufanyi vizuri akitolea mfano eneo la Elimu ya Msingi na Sekondari kuwa hali ya ufaulu hairidhishi ambapo Mkoa umeshika nafasi ya 24 kati ya Mikoa 26 kwenye matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi  mwaka 2017, Wakati kwa upande wa Matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya Sekondari kidato cha nne mwaka 2016 Mkoa ulikuwa wa 19 kati ya Mikoa 26..  

Amewataka Viongozi na Watendaji wote kwenye Wilaya za Mkoa wa Dodoma kutambua wana jukumu kubwa la kusimamia elimu kwenye Wilaya zao na ameagiza kila Wilaya ikae na kufanya tathimini ya sababu ya kufanya vibaya kwenye matokeo ya mitihani ya msingi na sekondari na kutafuta majibu ya changamoto hizo na pia kubuni mikakati itakayo ukwamua Mkoa kielimu na baadae mipango hiyo ya Wilaya ijadiliwe pamoja ili  kutoka na mkakati mmoja wa Mkoa wa kupandisha hali ya Elimu na Ufaulu kwenye Mkoa wa Dodoma.

Dkt. Mahenge amezitaka Wilaya za Mkoa wa Dodoma kujipanga vizuri kwenye Sekta ya kilimo akiainisha kuwa Viongozi na Watendaji kwenye Mkoa wana jukumu la kuhakikisha tatizo la upungufu wa chakula linakuwa historia kwenye Mkoa wa Dodoma kwa kuhimiza Wananchi wetu kulima mazao yenye kustawi hata katika mazingira ya maji kidogo na hali ya hewa ya Mkoa wa Dodoma kama Mtama, Uwele, Muhogo na Alizeti.

Aidha, Katika kukuza Mapato na Uchumi wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, Dkt. Mahenge amezitaka Halmashauri hizo kwa sasa kuanza uwekezaji kwenye kilimo cha Korosho ambacho kimewasaidia wakulima wengi kuinua hali ya uchumi kwenye maeneo wanayolima zao hilo, amesema tayari wataalamu wa kilimo wamebainisha kuwa zao hilo linauwezo wa kustawi vizuri na kuwa na mavuno ya kuridhisha kwenye Mkoa wa Dodoma na kiuchumi soko la Korosho lipo na bei ya zao hilo kwenye soko ni nzuri. Ameipongeza Wilaya ya mpwapwa kwa jitihada walizoanza za kuwekeza kwenye kilimo cha Korosho na amezitaka Wilaya nyingine Mkoani Dodoma kuona namna nazo zinavyoweza kuanza utekelezaji wa mpango huo wa kilimo cha Korosho

Dkt. Mahenge amezitaka Wilaya za Mkoa wa Dodoma kuweka mkakati wa utekelezaji wa Kampeni ya Serikali ya Uanzishaji wa Viwanda kwa kila Mkoa uliozinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Seleman Jaffo kwa kuzishirikisha hadi ngazi za chini kwenye wilaya zetu na kutaka mkakati huo ulenge kuanzisha viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazotokana na malighafi ya mazao yanayolimwa kwenye Mkoa wa Dodoma.

Aidha, ametaka Mkakati huo wa uanzishaji Viwanda kwa kila Wilaya uwajumuishe Vijana na Wanawake,  kwa kuwaagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Dodoma kuhakikisha wanatenga asilimia kumi (10%) kwenye bajeti zao za Halmashauri kwa ajili ya miradi ya uzalishaji mali na uchumi kwa vijana na wanawake, na fedha hizo zipelekwe kwenye kuanzisha viwanda vidogovidogo kwa ajili ya makundi hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mheshimiwa Jabir Shekimweri amemwelezea Dkt. Mahenge kuwa bado Makusanyo ya Wilaya hiyo hayaridhishi kwani kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Wilaya ya Mpwapwa ililenga kukusanya zaidi ya shilingi 2,800,000,000 lakini mapato halisi yalikuwa Shilingi takribani Bilioni moja, akibainisha kuwa hali hiyo inatokana na uchache wa vyanzo vya mapato hivyo ili kukuza mapato na hali ya uchumi tayari Wilaya ya Mpwapwa imeanza utekelezaji wa Mkakati wa kukuza kilimo cha Korosho.

 

“Kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho tayari Wilaya ya Mpwapwa tumepokea jumla ya tani sita (6) za mbegu bora na za muda mfupi za Korosho na pia tumefikia makubaliano na Bodi ya Korosho  ya kujenga kiwanda cha kubangua  Korosho hapa Mpwapwa jambo ambalo litakuza sana kilimo cha korosho na kuingizia Wananchi na Wilaya kwa ujumla pato kubwa na kukuza uchumi” alibainisha Mheshimiwa Shekimweri.

Mheshimiwa Shekimweri amesema tayari Wilaya ya Mpwapwa imeanza kuitikia Maelekezo ya Serikali ya kuanzisha Viwanda  na tayari Wilaya imetenga eneo la hekta 3.7 kwa ajili ya uanzishaji wa viwanda ambapo baada ya upimaji wa eneo hilo jumla ya viwanja 40 vilipatikana kwa ajili ya ujenzi wa viwanda,  hatua iliyopo kwa sasa ni kuliwekea eneo hilo la viwanda miundombinu muhimu kama barabara maji na umeme ili wadau mbalimbali waweze kujenga viwanda.

Pamoja na kuzungumza na Watumishi wa Serikali Wilayani humo, Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge alitembelea kitalu cha miche ya Korosho kwenye Gereza la Mpwapwa,alitembelea kituo cha utafiti wa Mifugo Mpwapwa, Mradi wa  kiwanda cha kukamua alizeti na kujibu kero za wananchi kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Chitemo.

 

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa