• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

“Zoezi la Anwani za makazi liende sambamba na upimaji wa viwanja”- RC Mtaka

Tarehe iliyowekwa: February 23rd, 2022

" Anuani za Makazi ziende sambamba na Upimaji wa Viwanja" RC Mtaka.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Anthony Mtaka amewashauri wananchi wa Kondoa Mji kuwa zoezi la anuani za makazi liende sambamba na upimaji wa viwanja ili kuweza kuleta matokeo chanya.

Ushauri huo ameutoa wakati wa kikao cha uzinduzi wa anuani za makazi pamoja na postikodi kilichofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

"Leo tunazindua anuani za makazi tujitahidi kumaliza zoezi hili kwa wakati ili ifikapo tarehe 19 Machi Rais wetu anamaliza mwaka mmoja wa uongozi hivyo basi ni lazima  tumpe zawadi kwa kumwambia Kondoa Mji tumemaliza zoezi hilo kikamilifu", amesema RC Mtaka.

Ameendelea kwa kusema kuwa anatamani Kondoa Mji ibuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitaisaidia Halmashauri kujiendesha yenyewe lakini pia amesema kuwa ili hayo yawezekane wanatakiwa kuhakikisha kuwa ardhi imepimwa tayari kwa matumizi mbalimbali.

"Ni vyema kuwa wabunifu kwa kuwa na vyanzo vingi vya mapato badala ya kutegemea vilevile ambayo haviwapeleki popote ifike mahali tufanye mageuzi kwenye Kata nane zenye mitaa 36 kwani uwezo mnao hamuendi kuroga mnafanya vizuri zaidi hivyo hakikisheni rasilimali yenu ardhi imepimwa na hakuna mtu anafanya shughuli za maendeleo kwenye ardhi ambayo haijapimwa", amesisitiza RC Mtaka.

Kwa upande wake Meneja wa Posta Mkoa wa Dodoma ndg Ferdinand Kabenela amesema kwamba nia ya Serikali ni kumsogeza mwananchi karibu na huduma za jamii na kumuwezesha kupata huduma anazostahili kwa uhakika.

"Anuani za makazi zipo katika ilani ya CCM lengo ni kuhakikisha kuwa watu wake wanapatikana wapi na wanaishi wapi hivyo tunapaswa kutambua makazi yako sawa upo Kondoa lakini unapatikana wapi", amesema Kabenela


Ameendelea kusema kuwa Postikodi ni mfumo maalum wa alama au tarakimu unaomtambulisha mtu anapoishi na kwamba anuani za makazi zina faida nyungi zikiwemo kuwezesha ununuzi wa bidhaa kwa njia ya mtandao, kuimarisha ulinzi na usalama pamoja na kurahisisha sensa za watu na makazi.

"Niwasihi wanakondoa mjitajidi kutoa majina ya mitaa yaliyorasimishwa ili kuondoa changamoto wakati wa kuingiza kwenye mfumo hivyo hizi taarifa zinatakiwa ziwe sahihi na ambazo hazibadiliki lakini pia sio tu kuweka miundombinu ya anuani hizi bali hata utunzaji wake hivyo wote tushiriki kikamilifu", amesisitiza Ndg. Kabenela.

Halikadhalika Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamisi Mkanachi amesema kuwa wamepokea vizuri zoezi hilo la anuani za makazi kilichobaki ni utekelezaji.

"Leo tunaenda kuzindua zoezi la anuani za makazi ambapo tuna kata nane na mitaa 36 na barabara 255 na mpaka sasa tumeweka vibao katika mitaa 76 nina imani kesho ya Kondoa itakuwa bora kuliko jana yake kuna siku Mkoa utajivunia Kondoa", amesema Dkt Mkanachi.

Hata hivyo akiongea awali Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Chacha amesema kuwa viongozi hawapaswi kuegemea upande wowote kwa kwa kufanya hivyo kunaleta matabaka na migogoro kazini badala yake wapaswa kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kwa manufaa ya wananchi

"Ni lazima tuwape nafasi ya kuwasikiliza wale tunaowaongoza ili tujue wana mtazamo gani na maoni gani juu yetu kupitia wao tutaweza kujua nini kinahitajika kiwe ushauri wangu tuwe wamoja ili tuweze kusonga mbele", amesisitiza Dc Chacha.

Kikao cha uzinduzi wa anuani za makazi kwa Halmashauri ya Mji Kondoa kimefanyika ambapo mgeni alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka  ambapo Kondoa Mji wameahidi kumaliza zoezi  hili kabla ya mwezi Machi ambapo kitaifa linatarajia kuhitimishwa ifikapo  Mei 30 mwaka huu.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa