• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Bilioni 3.7 za miradi ya maendeleo zapelekwa Kolo kwa miaka mitatu

Tarehe iliyowekwa: July 18th, 2024

Zaidi ya shilingi bilioni 3.7 za kutekeleza miradi ya maendeleo kuanzia mwaka 2021 hadi 2024 zimepelekwa katika kata ya Kolo Halmashauri ya Mji Kondoa zikiwa ni fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji, Elimu, afya na barabara.

Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Kolo Mhe. Iddi Ng’ungu mbele ya wajumbe wa kamati ya siasa mkoa, viongozi wa wilaya na wananchi wa mtaa wa Choka waliofika katika Zahanati ya Choka kujionea utekelezaji wa mradi huo hivi karibuni.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kututhamini sisi watu wa Choka na watu wa Kolo kwa kuwa ametuthamini na kusikiliza kilio chetu na kutuletea miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 3.7 na kwasasa kata nzima nimebakiza mtaa mmoja ambao hauna zahanati ila tumeanza kuchangishana nguvu kazi za wananchi ili kujenga zahanati hiyo,”amesema Mhe. Ng’ungu

Aidha ameishukuru serikali kwa kuwajengea Zahanati ya Choka ambayo imegharimu kiasi cha shilingi milioni 87 ikiwa shilingi milioni 75 ni fedha kutoka Serikali Kuu, shilingi milioni 9 fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri shilingi milioni 3 nuvu za wananchi na ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji

Akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Saidi Majaliwa amesema kuwa Halmashauri inatambua mchango wa wananchi na itaendelea kuwaunga mkono wajumbe wa kamati ya zahanati kutokana na kufanya kazi kwa kujitolewa na kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika na kuanza kufanya kazi mapema mwezi Agosti, 2024.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge amewaomba wananchi wa Mtaa wa Choka na kata ya Kolo kuwa na imani na diwani wa kata hiyo kwa kuwa ndiye anayewapambania kuhakikisha miradi ya miradi inaletwa katika kata yao.


“Mheshimwa Mwenyekiti kata hii ndio ambayo imepiga hatua sana kimaendeleo ni kata ambayo huduma zote muhimu zimefika zahanati zimejengwa mitaa yote bado mmoja, kituo cha afya, barabara zimefunguliwa, maji yameletwa na madarasa yamejengwa na huo mtaa mmoja tunaangalia kama Halmashauri katika bajeti namna gani tutawaunga mkono”amesema Mhe. Kiberenge

Akiongea awali Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma Ndg. Pili Agustino amesema anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwasaidia wananchi wa Choka kwa kuwasogezea huduma ya zahanati kwa kuwa walikuwa na changamoto ya huduma hiyo.

“Hata hivyo pia nawapongeza wote akiwemo mbunge, diwani, Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kusimamia miradi ya maendeleo na nimeongea na Mkurugenzi amesema atahakikisha huduma inaanza tarehe 1, Agosti 2024 na yote hiyo sababu wanawajali wananchi,”amesisitiza Katibu Pili.

Kwa upande wake mmoja wa wananchi wa Mtaa wa Kolo Ndg. Mary Mbaga amemshukuru Rais kwa kuwajengea zahanati katika mtaa wao kwani walikuwa wanapata adha kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya afya na walitumia gharama kubwa kusafiri ambapo kwasasa wanaamini wataipata hapohapo mtaani.

Kata ya Kolo ina mitaa 5 ambapo serikali imejenga zahanati katika mitaa 4 na kituo cha afya kimoja na hadi sasa wananchiwa mtaa mmoja wa Gubali uliosalia wameshaanza kutoa nguvu kazi za kujenga zahanati katika mtaa wao na wamechangia shilingi milioni tatu na michango inaendelea.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • "Sintamzibia ruhusa mtumishi anayetaka kwenda masomoni"- Mkurugenzi Majaliwa

    June 01, 2025
  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa