• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Fanyeni kazi kwa umoja na mshikamano kwa manufaa ya wananchi" - Mwenyekiti Kiberenge

Tarehe iliyowekwa: September 30th, 2021

Na. Leah  Joseph

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge amewaasa watumishi pamoja na viongozi ndani ya Halmashauri ya Mji Kondoa kuendelea kudumisha umoja na mshikamano katika kutekeleza shughuli za Serikali za kuleta maendeleo kwa wananchi.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao cha baraza maalum la kupitisha hesabu za mwisho za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Kondoa hivi karibuni.

"Sitaki kusikia kuna mgawanyiko wa makundi ndani ya Halmashauri ninayoiongoza ninachotaka ni kuona tunadumisha amani na mshikamano na tunafanya kazi kwa pamoja kwa sababu sisi ni wamoja na Kondoa ni ya kwetu sote" , amesema Mhe. Kiberenge.

Mhe. Kiberenge ameendelea kwa kusema kuwa ni wajibu wa kila mtu kwa nafasi yake kufanya kazi kwa bidii ili kuwaletea wananchi maendeleo na katika kufanikisha hilo ni vema kila mtu awe na hofu na utu ndani yake na kuachana na malumbano badala yake mwenye changamoto  ajibiwe kwa hoja na sio vijembe.

Halikadhalika Katibu Tawala Wilaya ya Kondoa Andrea Ng'wani amewaomba washiriki wa baraza hilo kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO 19 ambayo inatolewa bure bila malipo katika vituo vyote vya afya.

"Nitoe rai kwa watu wote  kuendelea kuwa mabalozi wa kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO 19 kwani ugonjwa huu  bado upo na unaua lakini pia ninaimani kuwa watanzania ni waelewa tuendelee kuwaelimisha hatimaye wote watachanja "amesisitiza Katibu Tawala.

Hata hivyo Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma Nathalis Linuma amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Mji Kondoa kwa jinsi walivyokuwa wanajibu hoja zilizokuwa zinawasilishwa na Waheshimiwa Madiwani ambapo amewashauri kuzifanyia kazi hoja ambazo hazijakaa sawa ili kuepuka kupata hati chafu.

"Mnaonekana mlivyo makini sana kwani nimeona jinsi mlivyokuwa mnaweka vitu sawa kwa hilo hongereni sana ninaimani kupitia Mkurugenzi wenu mtakaa na mtajadili hoja zenu vizuri na kuziweka sawa mapema ili baadae ziweze kule matokeo mazuri na hatimaye Kondoa ipate hati safi kama ilivyokuwa mwanzo" ,amesisitiza Linuma

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa Mohamed Kova amesema kuwa ni lazima kila mtu kwa ujuzi wake alionao afanye kazi kwa bidii bila kuona haya wala kuogopa vitisho kwa ili kuhakikisha Halmashauri inasonga mbele.

"Nilazima Viongozi, Wataalamu na wananchi tuwe kitu kimoja kwa kufanya hivyo mafanikio yatapatikana hivyo  basi zingatieni ufanisi ili kuzitendea haki taaluma zenu mlizosomea na mtu akifanya vizuri asijisifie bali angoje asifiwe ili apate moyo wa kuendelea kufanya vizuri zaidi" , amesisitiza Mwenyekiti Kova.

Kikao cha baraza maalum la kupitisha hesabu za mwisho za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kimefanyika kikiwa na lengo la kuwasilisha na kujadili taarifa hiyo ambapo kilihudhuliwa na Waheshimiwa Madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Menejimenti pamoja na Wananchi.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Wasira aelezea faida za Muungano kwa wananchi wa Kondoa

    April 26, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa