• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji wapongezwa kutoa mikopo ya asilimia 10 awamu ya pili

Tarehe iliyowekwa: February 19th, 2025

Uongozi wa Halmashauri ya Mji Kondoa umepongezwa kwa kuhakikisha adhma ya serikali ya kuwezesha wananchi kiuchumi inafanikiwa baada ya kutoa mikopo itokanayo na asilimia 10 ya mapato yenye thamani ya shilingi milioni 168.9 kwa awamu ya pili.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa wakati wa hafla ya kukabidhi hundi zenye thamani ya shilingi milioni 168.9 na pikipiki 20 kwa vikundi 19 vilivyopata mkopo iliyofanyika katika viwanja vya Stendi ya Zamani.

“Niwapongeze Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa kwa kutoa leo milioni 168 ndani ya miezi mitatu baada ya ile mikopo ya awali na kufanya jumla ya zaidi ya shilingi milioni 360 kutolewa kwa vikundi 36 hizi ni fedha nyingi kwa halmashauri inayokuwa kama Kondoa Mji hongereni sana,”amesema Mhe. Nyangasa

Aidha amewaasa wanufaika wa mikopo hiyo kuhakikisha kuwa inakwenda kutekeleza lengo kusudiwa na si vinginevyo ikiwa ni pamoja na kufanya marejesho kwa wakati ili kukuza mfuko wa mikopo na kuwanufaisha waombaji wengine ili nao wainuke kiuchumi na kujitengemea.

“Lakini katika harakati za kutafuta maisha kuna mengi nawaomba mkajiepushe kuchukua mikopo katika taasisi zinazoibuka ambazo zinatoa mikopo inayowaumiza wananchi na serikali kuliona hili ikatoa mikopo hii hivyo tuitumie vizuri fursa hii ya mikopo inayotolewa na kutumia taasisi rasmi kukopa fedha ili kuepuka usumbufu hapo baadae”amesisitiza Mhe. Fatma

Ameongeza kwa kuzishauri taasisi za fedha kuanza kuibua mikopo yenye masharti nafuu ambayo wananchi wanaweza kunufaika ili miaka mitano ijayo mabadiliko yaonekane na kusema kuwa hana mashaka na vikundi vilivyokopeshwa kwa kuwa vimepitia michakato yote muhimu kabla ya kupewa mkopo.

Akitoa taarifa awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Said Majaliwa amesema Halmashauri awali wametoa shilingi milioni 197.7 kwa vikundi 17 na sasa imetoa shilingi milioni 168.9 kwa vikundi 19 ambapo jumla ya shilingi milioni 366 kwa awamu mbili.

“Mhe. Mkuu wa Wilaya leo tumetoa shilingi milioni 168.9 kwa vikundi 19 ambapo kati ya hivyo vikundi 9 ni wanawake, 7 vijana na 3 ni watu wenye ulemavu na wamepata fedha zao kupitia benki zetu za CRDB na NMB, lakini pia Halmashauri tumeendelea kutoa zabuni kwa vikundi tulivyoviwezesha ikiwemo kikundi cha Mwangaza”amesema Mkurugenzi Majaliwa

Ameendelea kueleza kuwa Halmashauri itaendelea kutenga fedha na kuvikopesha vikundi vyote vitakavyokidhi vigezo na kuendelea kuwapatia zabuni katika miradi inayoendelea ili kuhakikisha wanufaika wananufaika na kuukuza mji wa Kondoa.

Akiongea kwa niaba ya wanavikundi Ndg. Philipo Chonya amesema wanaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaona vijana wa bodaboda na kuwapatia pikipiki kwa kuwa walikuwa wakipata shida katika pikipiki za mkataba walizokuwa wakifanya awali na kuahidi kurudisha mikopo kwa wakati.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa