• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji washauriwa kutumia kanuni na Mbegu bora za alizeti

Tarehe iliyowekwa: January 26th, 2022

Na: Leah Joseph - Kondoa

Afisa Kilimo Mkoa waDodoma Bw.Benard Abraham amewashauri wakulima wa alizeti ndani ya Halmashauri ya Mji Kondoa kutumia mbegu bora za alizeti ili kupata mazao mengi yenye tija na yatakayowaletea faida kubwa.

Ushauri huo ameutoa wakati wa mafunzo ya kuinua kilimo cha alizeti na namna bora ya kupanda zao hilo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mpalangwi hivi karibuni.

“Kila zao ama mmea unaopandwa una nafasi yake inayotakiwa kupandwa na ndio maana leo hii tupo hapa kuwafundisha namna bora ya upandaji kwa kuzingatia aina bora ya mbegu lengo ni kupata mazao mengi yatakayotuletea faida”amesema Bwana Bernard.

Aidha ameendelea kwa kusema kuwa wakulima wanatakiwa kupanda kwa kuzingatia nafasi ambazo wameelekezwa na wataalam kwakuwa mavuno mengi yanategemena na wingi wa mimea hivyo wakulima waache kulima kwa mazoea na kulalamika kuwa soko ni baya badala yake waongeze juhudi na kulima kwa tija.

“Hii shughuli ya kilimo ambayo tunayoifanya inatughalimu pesa nyingi nguvu na muda wetu hivyo basi ni lazima tuifanye kwa usahihi na kwa wakati kwani tukienda kinyume na hapa inatupeleka kwenye umaskini na hasara kubwa”amesisitiza Bwana Bernard

Kwa upande wake Afisa Kilimo Halmashauri ya Mji Kondoa Hassan Kiseto amesema kuwa huu ni mpango wa kilimo cha alizeti kwa mikoa minne ya kipaumbele wenye lengo la kupunguza uhaba wa mafuta ya kula nchini ambapo Mkoa wa Dodoma ni mmojawapo na kwamba Waziri mwenye dhamana ameichagua Halmashauri ya Mji Kondoa Kata ya Suruke ambapo atakuja kuzindua mpango mkakati wa uzalishaji wa zao la alizeti.

“Katika Halmashauri ya Mji Kondoa Serikali imeona na sisi isituache bure hivyo basi imetuletea mbegu kwa bei ya ruzuku ambayo kila mwananchi anaweza kuimudu shilingi 3500 kwa kilo ambapo tulipokea tani 11 lakini mpaka sasa tumeuza tani 4 bado tani 9”ameongeza Hassan Kiseto.

Halikadhalika ameendelea kwa kusema kuwa itakuwa siyo vyema Wizara kutoa mbegu alafu zibaki hivyo ametoa wito kwa wakulima wote kuchangamkia fursa hii kununua mbegu zote na kuzingatia upandaji wa kisasa kwani mpaka sasa Serikali haina mpango wa kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi lengo ni kuwainua wakulima wa ndani wa alizeti kuuza mafuta yao kwa bei nzuri ili wapate faida na kuondoa tatizo la uhaba wa mafuta ya kula nchini.

Hata hivyo Afisa Ugani Kata ya Suruke Bi.Hamida Ramadhan amewaambia wakulima wa alizeti namna bora ya upandaji wa zao la alizeti ikiwa ni pamoja na kufuata sm 30 shimo kwa shimo na sm 75 mstari kwa mstari hii ni kwa mbegu moja na sm 60 urefu na upana sm 75 kwa mbegu mbili na shimo linatakiwa kuchimbwa sm 7 na mbolea inayopendekezwa ni Yala otesha na Dapo.

“Wakati wa kupanda sio lazima utumie mbegu ya dukani unaweza kutumia samadi na ndio maana tunawashauri kuanza maandalizi ya mashamba mapema lengo ni kupata mazao mengi yenye faida”amesisitiza Bi. Hamida.

Mafunzo ya mpango wa kilimo cha alizeti yamefanyika ambapo yamehudhuriwa na wataalamu wa kilimo toka Wizara ya Kilimo,Maafisa Kilimo ngazi ya Mkoa na Halmashauri, Maafisa Ugani na wakulima.



Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa