• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkurugenzi aiongoza Menejimenti kusikiliza kero Kingale

Tarehe iliyowekwa: May 29th, 2024

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Said Majaliwa amewaongoza wajumbe wa Timu ya Menejimenti kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata ya Kingale ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kauli mbiu ya mkoa ya Kero yako,wajibu wangu.

Kazi hiyo imefanyika katika Ofisi ya kata ya Kingale ambapo pia ilihusisha wataalam wote wa kata ya Kingale ikiwa ni siku ya kwanza kati ya siku tatu za ziara ya kata kwa kata itakayofanywa na Mkurugenzi na Wakuu wa Idara.

Akiongea na wataalam wa kata ya Kingale wakati wa kuhitimisha zoezi hilo Mkurugenzi amewataka Maafisa Watendaji wa Kata kuiga mfano huo kwa kutenga angalau siku moja kwa wiki kufika katika mitaa yao na kusikiliza na kutatua kero za wananchi badala ya kukaa ofisini.

“Mtoke mkawasikilize wananchi kero iliyo nje ya uwezo wenu ileteni Halmashauri ili tuitatue tusiwaache wananchi wakakaa na changamoto zinazoweza kutatulika na usiende peke yako wabebe na wataalam wote waliopo ngazi ya kata mkawahudie wananchi,”amesema Mkurugenzi Majaliwa

Aidha ameahidi kuendelea kuwawezesha watendaji fedha kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi za mitaa ili waweze kufanya kazi ya kuwahudumia kwa ufanisi zaidi wananchi na kuwataka watendaji wasiokaa katika maeneo yao kurudi katika maeneo yao.

“Kero zote tumezipatia majibu isipokuwa za TARURA na TANESCO tumezichukua na tutaziwasilisha kwa wahusika kwa ajili ya kupata ufumbuzi na majibu tutayarudisha kwenu mhakikishe wananchi wanapata mrejesho huo”amesisitiza Mkurugenzi Majaliwa

Ameendelea kuwataka Watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha wanahamasisha kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura zoezi linalotarajia kuanza hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Awali wananchi wa kata ya Kingale wamewasilisha changamoto kubwa zinazowakabili katika kata yao kuwa ni pamoja na kukatika mara kwa mara kwa umeme, changamoto ya kukosekana kwa mawasiliano ya simu kwa baadhi ya maeneo na upatikanaji wa maji ya uhakika.

Mkurugenzi na Wakuu wa Idara wamepata fursa ya kusikiliza kero na kuzitatua zilizo chini ya Halmashauri na kuzichukua zingine kwa ajili ya kuziwasilisha katika ofisi husika kwa ajili ya kupata ufumbuzi ambapo wamefanikiwa kuwasikiliza wananchi wote 20 waliojitokeza na zoezi liaendelea kwa mwezi huu kwa kata ya Kondoa Mjini na Kilimani.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa