• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mafundi ujenzi na wanawake wajasiriamali wapigwa msasa mfumo wa NEST

Tarehe iliyowekwa: July 20th, 2024

Mafundi ujenzi zaidi ya thelathini na wanawake wajasiriamali katika Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kuhakikisha wanajisajili na kulipia ada ya mfumo wa manunuzi ya serikali ili kupata fursa mbalimbali za kimanunuzi zinazofanywa na Halmashauri.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kondoa na kufunguliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa hivi karibuni.

Akiongea wakati wa kikao hicho Mkurugenzi amewataka washiriki wa kikao hicho kujiamini kwani uwezo wa kufanya kazi wanao yeye atahakikisha wote wanapata kazi zitakazotangazwa na Halmashauri kupitia mfumo wa manunuzi wa serikali ambao unawataka wao kujisajili kwanza.

"Serikali imeleta fedha nyingi za miradi katika Halmashauri Chandimo madarasa, Kingale shule nzima ya ufundi, Gubali mabweni, Bolisa nyumba ya mwalimu, Tura day madarasa, Ula Sekondari madarasa, Unkuku madarasa hapo kweli kuna mtu atakosa kazi kweli ya kufanya ila msipojisajili hamuwezi kupata kazi hizo,"amesema Mkurugenzi Majaliwa

Aidha amewaeleza kuwa mfumo huo umekuja kwa ajili ya kuondoa malalamiko mengi yaliyokuwa yakitolewa na mafundi ya kuombwa rushwa ili wachaguliwe na kupewa kazi kwani kwasasa kila kitu kinafanyika kwenye mfumo hivyo ni vigumu wao kuombwa rushwa.

Hatahivyo amewataka mafundi hao kuwa wawazi kuelezea changamoto zozote wanazokabiliana nazo wakati wa utekelezaji wa miradi katika Halmashauri ya Mji Kondoa ili miradi ikamilike kwa wakati uliopangwa.

Aidha amewataka wanawake wajasiriamali waliojitokeza katika kikao hicho kujiunga katika vikundi na kujisajili katika mfumo wa manunuzi ya serikali ili kupata fursa mbalimbali za kazi zitakazotolewa na Halmashauri.

"Wanawake mna fursa nyingi kwasasa Halmashauri inatarajia kutangaza kazi ya usafi wa ofisi yake na ufagiaji wa barabara ili kuuweka mji katika hali ya usafi sasa ili fursa zisiwapite mjisajili kwenye mfumo huo,"amesisitiza Mkurugenzi Majaliwa

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa kitengo cha Manunuzi Ndg. Emmanuel Wambura amewaambia washiriki hao kuwa milango ipo wazi wakati wowote kwa wote ambao watahitaji msaadavwa kujengewa uwezo katika kujisajili ambapo wengi wamejisajili hivyo wamalizie kulipa ada ya usajili ili wapate fursa zitakazotangazwa.

Kwa upande wao mafundi wameishukuru Halmashauri kwa kuwapatia elimu hiyo na kuahidi kulipia ada ya usajili ili fursa zitakazotangazwa wasizikose a kuomba changamoto walizokuwa wakiabiliana nazo awali zirekebishwe kama ilivyoahidiwa.

Kikao hicho kimefanyika kwa ajili ya kuwajengea uwezo washiriki ambao ni mafundi ujenzi na wazabuni na wanawake wajasiriamali wanaojishughulisha na utengenezaji wa sabuni na usindikaji wa vyakula ambapo kanuni ya manunuzi ya umma 2024 inazitaka taasisi kuwapa fursa watu wa makundi maalum ya vijana, wanawake n watu wenye ulemavu.

Matangazo

  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Kondoa Mji watoa mafunzo kwa vikundi 16 vya mikopo awamu ya tatu

    June 24, 2025
  • Wataalam wa Kilimo na Mifugo Kondoa Mji watembelea Nanenane Jijini Dodoma

    June 24, 2025
  • Watumishi watakiwa kuendelea kutoa elimu ya stakabadhi ghalani

    June 23, 2025
  • Baraza Maalum Kondoa Mji lapitisha Sheria ndogo kuimarisha vyanzo vya mapato

    June 20, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa